Viboko ni njia mbadala wa kutoa elimu bora hapa nchini?

Joined
Mar 15, 2013
Posts
24
Reaction score
9
Hivi majuzi nimemsikia Naibu waziri wa elimu mh.Philipo Mulugo akisema kwamba serikali inanuia kurejesha adhabu ya vibo shuleni ili kurejesha nidhamu kwa wanafunzi na kuwafanya watulie kujisomea.

Maswali yangu kwa Naibu waziri:

1. Kilichochochea mpaka adhabu za viboko ziondolewe na walimu kupewa masharti magumu katika kutoa adhabu za viboko shuleni kimekwisha?

2.Mataifa wahisani tumewapa kipaumbele katika kuingilia mambo yetu hata ya ndani ya nchi ikiwemo na masuala ya elimu kiasi kwamba yapo mambo ambayo hutulazimisha kuyafanya kwa matakwa yao, je, tumejipanga sasa kuamua mambo yetu wenyewe na kuachana na muzimu wa kuzungusha bakuli kwa hao wahisani?

3. Adhabu ya viboko inaumiza wote yaani anayepewa adhabu(mwanafunzi) na anayetoa adhabu hiyo(mwalimu) kwani mwalimu lazima atumie nguvu nyingi kumwadhibu mwanafunzi. Je, mnao mkakati wa kumboreshea maslahi walimu ili wale, wanywe washibe na wakidhi mahitaji yao ya msingi kuwa tayari kukabiliana na shughuli hiyo?

Binafsi nina asilimia ndogo kuamini kwamba adhabu za viboko ni mbadala wa kuboresha elimu hapa nchini isipokuwa naona kuna ukwepaji wa kutimiza mambo ya msingi ambayo yakifanyika tu moja kwa moja lazima elimu bora itolewe.

Baadhi ya njia mbadala na za makusudi ni hizi hapa:

1. Serikali iwalipe mishahara inayokidhi na kuendana na gharama za maisha.
2.Walimu walipwe mishahara sawa na watumishi wengine ili kuondoa kinyongo kilichojificha kwenye vichwa vya walimu.
3. Walimu walipwe posho kama zilivyo kada zingine za utumishi kwa ajili ya kuwapa motisha ya kazi walimu.
4. Serikali kupitia wizara ya elimu ihakikishe vifaa na zana kwa ajili ya ufundishaji na ujifunzaji vinapatikana kwa kila shule ikiwemo maabara kwa shule za sekondari.
5. Mazingira ya kufundishia na kujifunzia yaboreshwe lwa kupewa miundo mbinu zinazohitajika.
6.Sheria zote kandamizi ziondolewe na walimu wapewe mamlaka ya kamili ya maamuzi shuleni tofauti na kuendeshwa na maofisa ambao baadhi yao weleldi wao huonekana mdogo.
7.Walimu washirikishwe kwa kila jambo linalohusu elimu yetu.Wapewe semina, warsha na kupewa fursa za kujiendeleza bila ubaguzi wowote.
8. Baraza la mitihani libadilishe mifumo ya utunzi wa mitihani ambayo haina tija hususani kwa shule za misingi na mitihani ya sekondari inahitaji maboresho.

Haki ya nani nkwambia Mh.Mulugo mkifanikiwa kutekeleza haya Walimu watafanya kazi usiku na mchana hata ziku za mapumziko mtawakuta madarasani.

Au wewe mdau wa elimu unasemaje

 
Waalimu tuliambiwa na kiranja mkuu kwamba akili zetu tuchanganye na za kuambiwa sasa ndio tupo kutengeneza huo mchanganyiko ili kupata kemikali kaka. kumbuka uwajibikaji wa mwalimu unabeba asilimia kubwa sana ya ufaulu wa mtoto.
 
JOSPIDE MAJABA
1. Kilichochochea mpaka adhabu za viboko ziondolewe na walimu kupewa masharti magumu katika kutoa adhabu za viboko shuleni kimekwisha?

Mkuu, na wengine wanatumikia vifungo kwa kesi ya kupiga wanafunzi viboko. Hivi watawafutia adhabu? Walimu hawana maslahi yeyote kupiga wanafunzi viboko. Kwanza ni adhabu inayoleta uchungu sana. Ni lazima uwe katili sana "sadist" ili uweze kuitumia. Mhe Mulugo asitafute visingizio. Arudishe PTA (Parent-Teacher Associations) ili wazazi na walimu wawe na msimamo mmoja katika kulea wanafunzi. Mtindo wa kuwa na Kamati za Shule au Bodi za Shule bila PTA ndio unaosababisha walimu kuandamwa na wazazi kila mara walimu wanapotaka kuwaadabisha wanafunzi. Kuna sehemu nyingi tu walimu wamewahi kushambuliwa na wazazi kwa mambo kama hayo na Kamati za Shule wakiangalia. PTA ni forum ya kurekebishana. Kwanza kama kuna PTA si lazima mwalimu amchape mtoto wa mtu. Anaweza kuitwa mzazi aje yeye mwenyewe kumchapa mtoto wake mbele ya wenzake. Afu mambo ya kuchapana ndipo mtoto asome ndiyo nini hiyo? Siyo ujima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…