Vibosile vikwazo kwa wapendanao wenye mapenzi ya dhati

Vibosile vikwazo kwa wapendanao wenye mapenzi ya dhati

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Amani iwe nanyi wapendwa katika bwana,

Husika na kichwa hapo juu kinavyosomeka,

Vibosile huwa ni vikwazo sana kwa wapendanao.

Unaweza ukawa na msichana wako mkali tu tena mnapendana kinoma lakini likatokea jitu lenye mihela yake na kuanza kumfukizia huyo msichana kwa magari tofauti tofauti Leo mara liende na prado kesho mara tena limuibukie na Mark x yenye rangi nyeusi kali kinoma.

Jamaa haliishii hapo kila siku linampelekea maposho posho na makosho kosho hata kama hajaomba hata sent lenyewe linajaza malaki malaki kwenye tigo pesa yake.

Msichana wangu kuna likibosile limemufukuzia likaninyang'anya.

Hata kwa wanawake ni hivyo kama likitokea lijimama likaanza kumfukizia mmeo lazima akusahau aisee.


Vibosile siyo watu wa kimchezo mchezo

LONDON BABY
 
Hivi bado kuna mapenzi ya dhati?
Au huwa tunaadhimisha tu., kama mapinduzi day.
 
nawe una fursa ya kuwa kibosile, machungu uliyoyapata kwa kunyang'anywa demu ungeyatumia kama hamasa ya wewe kutafuta pesa kwa udi na uvumba, siku hizi hakuna huruma katka mapenzi inabd ujipange ndugu
 
Mkuu pambana na hali yako mwenzako alipambana
 
Mapenzi bila ela utabaki kuwa mpenzi mtazamaji tu☺☺
 
Back
Top Bottom