Elections 2010 Vibweka vya Uchaguzi Igunga: Mabasi kukamatwa, masanduku kwa DC na mengineyo..

Kama watoto wadogo vile,ovyo sana.
 
Huyo bwana yako sabodo ni kada wa c.c.m kuliko wewe lakini anakubali sera za cdm sembuse wewe chokest soda anasa! Kwee kwee kwee!! Kweli wewe pust.
 

Daah! yani unafikiri sana mzee!!
Kama unatoka shinyanga mjini Tinde ni juction! ukinyoosha unaelekea nzega/tabora au igunga na iwapo utakara kulia utaelekea kahama/kagera rwanda au burundi! radio uhuni wanauhakika gani kuwa walikuwa wanaelekea Igunga na si burundi au rwanda any way ni ile ukitaka kuumua mbwa mpe jina baya! wamegota ccm hizo trik zao zimeshastukiwa siku nyingi.
 
Hii redio haina tofauti na ile ya Rwanda, CCM, Vyombo vya habari na baadhi ya Wana habari iko siku watalipia vitendo vyao.
Mkuu, unajua yalianza hivihivi kule Ruanda??!!!
Hawa CCM wana akili timamu kweli?? haya mambo wanayoyapandikiza kwa watanzania ni kwa gharama za nani??
 

Mkuu Ntamaholo una hasira sana na hawa Magamba: any way usijali mkuu Mungu yupo nasi wapenda mabadiliko
 
Angalau tungejaribu kuutafuta ukweli wake halafu tungejadili kwa ukweli wake au uongo wake. Tatizo hapa ni kwamba nature, mazingira na source ya habari haviaminiki. Na mkishamfahamu mtu kuwa ni mwongo, hata akisema ukweli, hamuwezi kuamini!

kweli kabisa.
 
Radio uhuru ya sisiem, hzo ndio siasa zao za kuchochea!
 

Unategemea nini kama ndio hiyo radio, Ni uongo tu huo. Labda ni hao hao watu wa kijani ndio wanafanya hivyo. Bora ungelala kuboresha afya yako kuliko kusikiliza hiyo radio.
 
Kama ingekuwa ni kweli CCM wasingekaa kimya bila kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kwani hiyo ingekuwa turufu yao kubwa kwa ushindi wa Igunga. Jambo baya lolote la CDM polisi wangelitangaza haraka sana, so far huo ni uzushi na upuuzi tu.
 
Kuna kila sababu ya kutokuwa na wasiwasi na madai ya Mbowe. Kitendo cha jimbo la Igunga kuhamia Chadema CCM wanakitafsiri kama bonge la pigo kwao, aibu kubwa, na alama ya kudhoofika kwa chama chao kwamba inawezekana hali ikawa mbaya zaidi 2015.

Kwa kuzingatia hilo hawataki kufanya bahati nasibu ya uchaguzi halali kupitia ushindani halali. Na wapo tayari kuua kuhakisha Mbunge anatoka CCM. Niia ya kuiba kura wanayo, uwezo wa kuiba kura wanao na sababu za kuiba kura wanazo. Kwa upande wa Chadema, jukumu lao ni moja tu nalo ni kumpinga adui kwa kila namna. Vijana wa Chadema wako Nzega tayari kufatilia hayo masanduku ya kura.

Na kama Mbowe alivyosema..."wana Igunga wasiwe na wasiwasi hakuna kura ya mtu itakayoibiwa, tumejipanga kisawasawa, tutapambana nao mpaka kieleweke."
 
Kutoka hii radio usitegemee tofauti na ulichokisikia mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…