Elections 2010 Vibweka vya Uchaguzi Igunga: Mabasi kukamatwa, masanduku kwa DC na mengineyo..

Kelele za mwizi huyooo nazo zinasaidia yale masanduku ya Tunduru kama siyo kelele walikuwa wamepanga Kikwete ashinde kwa kishindo cha 80%.
 
Hivi kweli, inakuja akilini kweli. Ninavyojua mawakala wote wanakagua maboksi yote kabla ya watu kuanza kupiga kura. Hizo kura bandia si wataziona?
Hizi kelele zinatuchosha, wajaribu kufikirisha ubongo.

kura sikisha pigwa vituoni na kuhesabiwa vinapelekwa kwa msimamizi wa uchaguzi [mkurugenzi ] hapo ndipo wanapochakachuwa kuingiza hizo kura hewa...swali langu kama zimehesabiwa kituoni wanahesabu nini tena ? mara nyingi matokeo ya vituo yanakuwa tafauti na ya mkurugenzi
 

Bukijo,Pole kwa kuharibiwa moody yako asubuhi.
Naomba nikupe taarifa kamili:

Kuna wadau na wapenzi wa mageuzi au washabiki wa chama cha chadema ambao waliamua wao wenyewe kwenda kuwapa moyo na kutia hamasa kwa wanaIgunga,watu hao wametokea mwanza na walikuwa ndani ya Costa 4 idadi yao inafikia 120 hivi.watu hao walikamatwa jana saa tano usiku.

Nikweli polisi wamewakagua na kuchukua maelezo yao,watu hao hawakukutwa na silaha zozote wala aina yoyote ya rungu inasemekana walitaka kuwabambikia vitu hivyo,lakini vijana hao wakawa wajanja baada ya kukataa kuondoka usiku walipoachiwa.wameondoka asubuhi na hakuna tatizo.
 

Ya kule Tunduma bado ni fumbo. Kwanza tunapaswa kujiuliza ni nani aliyethibitisha kuwa mzigo ulikuwa ni vipodozi, utaambiwa RPC. Je palikuwa na upekuzi huru ama ndio wale wale walitumwa na magamba? Si jambo la uongo kuwa kura nyingi feki ziliingizwa mwaka jana. Yale maeneo ambayo nguvu ya umma haikuwa na nguvu sana, kura hizo zilipenyezwa na kuchakachua uchaguzi wa wananchi, yale maeneo ambayo kura zililindwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, Iringa, Musoma, Ubungo, Kawe na sehemu zingine hawakuthubutu.

Wana Igunga na CDM kwa ujumla hawa CCM wanaweza kufanya jambo lolote, hivyo hakuna kulala, hao vijana walitumwa Nzega iwe man to man, wakabe mpaka penalt ili CCM wakimbie kama walivyokimbia Tarime.

Mungu ibariki Tanzania. We are longing for a second liberation of our country.
 
Jamani wa TZ kuna haja sasa ya kuingia msituni kwa ajili ya kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi kwa MAGAMBA serius...!Without doing so hayo mabadiliko tunayohubiri kila siku kua tunayataka yatakua ni ndoto

BBJ mimi nakubaliana nawe asilimia 100. Nimewahi kuandika sana humu kuwa CCM kamwe haiwezi kutoka kwa sanduku la kura, zinahitajika nguvu. Wakuu CDM mkitoka Igunga itisheni maandamano Dar kuipinga CCM, Taifa sasa limeiva kwa ukombozi, hakuna haja ya kupoteza muda. Tufanye kama Libya maandamano kisha mtutu mpaka watokomee.
 
Mbowe si kasema washapeleka vijana wao Nzega, we kazee vipi...!!
 
Ukiona kutapatapa kwa hvi basi tambua tayari mjusi kabanwa na mlango ...mie niko tabora na kwa habari ninazozipata ni kwamba magamba wako hoi zaidi ya kawaida,mlioko mbali msipende kuamini baadhi ya vyombo vya habari kwa sasa kwani 90% ya mnayoletewa ni chakachuzed news contrary to what is just happening in the battle field...na CDM ikiweza kudhibiti wizi wa kura tu tayari itakuwa imeshinda
 
Hivi kweli, inakuja akilini kweli. Ninavyojua mawakala wote wanakagua maboksi yote kabla ya watu kuanza kupiga kura. Hizo kura bandia si wataziona?
Hizi kelele zinatuchosha, wajaribu kufikirisha ubongo.

Umeshawahi siki ndude inaitwa KITUO HEWA?
 
Hwa tumewazoea, huwa hawashindi kiuhalali kabisa, cku zote lazima waibe, but this tym Igunga kitanuka. Hatukubali tena..lazima tuige mfano wa wenzetu wa Ubungo na Arusha
 
Mchezo huwa hivi,

Kura zitahesabiwa vituoni lets say chama pinzani mnapata 250 na CCM 200, mnaanza kushangilia, masanduku yanakusanywa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambapo kura bandia zinaingizwa, mgombea wa CCM au chama kidogo kilichoandaliwa na CCM kinajidai kulalamika turudie kuhesabu, huku nje wapinzani tayari wanashangilia, baada ya kurudia kuhesabu inaonekana kumbe CCM wana kura 300 hapo kura 100 zimeongezwa na mchezo unakwisha. Mara nyingi unapoona sehemu wanachelewa kutangaza juwa zoezi hili linafanyika kwa usiri mkubwa. Ilitokea Busanda CDM wakaanza kushangilia baadae wakaambiwa kura za vijijini zilikuwa hazijafika, ilitokea pia Shinyanga, Segerea na sehemu zingine, safari hii Ubungo ilishindikana kutokana na uimara wa mawakala kila kituo kilikuwa na mawakala wa CDM zaidi ya wawili.

Kitu cha kufanya kwa sababu wanaofanya biashara hii ni binabamu kama sisi ni kuweka waangalizi sehemu yalipo masanduku kuanzia siku ya kuletwa yakiwa matupu, mbali ya mawakala kuwepo kila kituo kuwe na watu tofauti wakufatilia mienendo ya masanduku usiku na mchana toka yalipohifadhiwa, usafirishwaji, upigaji kura, kuhesabu kura na utunzwaji baada ya kuhesabu hadi matokeo yatangazwe na wawe na mawasiliano ya haraka linapotokea tukio lolote lisilo la kawaida.

Mwisho njia zote za kuingia na kutoka Igunga na kwenye Halmashauri zijulikane na wawe na waangalizi usiku na mchana, wakidhibiti mianya hiyo nina uhakika matokeo yatakayotangazwa yatakuwa halali.
 
Yale yale ya MKAMA aliyesema kuwa kuna makomandooooo, yaani siasa za Bongo inabidi Mungu aingilie sana
..Na kale kazee Wilson Mkama sioni tofauti yake na Makamba...Sijui CCM hawa watu huwa wanawatoa wapi?
 
Asante sana kwa taarifa!
 
Hivi kwa nini NINI GREAT THINKER a-tune redio uhuru jamani unajua itakuwa inakuharibia siku just kama KIBONDE na Clouds yake!!!!!!!!!!!!!

Samahni lakini ASHAKUM SI MATUSI!
 

you are right bro.

kinachotakiwa ni kuwa na usimamizi imara tangu kwenye zoezi la kuhesabu kura kule vituoni na baadae kuyalinda masanduku ya kura kuhakikisha hakuna wa kuingia ovyoovyo. hila za CCM zitashindwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…