Vichaa huona nini?

Na yule aliyevuta bangi kwa mara ya kwanza akawehuka huwa anaona nini?
 
Mshana Jr....hii si Mada ya kuweka/kuanzisha na kufanya ama kuwaacha wana JF na Tafakari...!!

Hii ni Mada PANA na NZITO (hasa kwa watu WAJUVI na WAZAMIVU wa mambo)

Ni vyema UKAINGIA Deep (ndani zaidi) katika kuzungumzia hali na matukio yanayo mkuta mtu huyu, na kwa kiasi fulani, unaweza kukuta unawasaidia Ndugu na Rafiki wa WAHANGA, kufahamu na kuchukua hatua namna ya ku-deal na watu jamii ya WAENDA WAZIMU (Lunacy)..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante mkuu kwa kutukumbusha jambo tupo wengi sana tunaozani busara za kichaa ni kutembea peku...Kumbe nyuma ya panzia kuna mengi sana tusioyajua..Kabla hujafa hujaumbika.
 
Kila mtu ana kichaa cha aina yake katika dunia hii, nadhani hakuna asiyekichaa kwa kiwango fulani..

Wengine wana kichaa cha kujilimbikizia mali.. Yani huyu hata awe na mshahara wa million 45 kwa mwezi ni lazima bado atajitahidi kila mwezi aibe million 40..

Wengine wanakichaa cha kuwahi makazini japokuwa wamechelewa kuamka.. Huyu utakuta umesimama ili kuwasaidia watu wavuke barabara lakini yeye bila kujali atajaribu kukupita na wakati anaona kabisa umesimama watu wavuke..

Wengine wana kichaa cha kuwa na wanawake/wanaume wengi.. Hawa utakuta ameoa/kuolewa lakini nje ana michepuko 25..

Vichaa wapo wengi sana..
 
Msongo waawazo, magonjwa hasa homa Kali, ajali, urithi. Ni baadhi tu vitu ya vitu vinavyosababisha mtindio wa ubongo au ugonjwa wa akili.
Wapo waliopitiliza hawa wanalala tu no kumgeuza , kumlisha, kumuogesha kila kitu umfanyie. Hawa Mara nyingi wanakua na utindio wa ubongo sio ugonjwa wa akili.
 
Nafikiri wanaona vitu ambavyo hatuvioni. Siku moja kicha kapita karibu na mama ntilie akiyekua anauza sana, akakaa pembeni akicheka sana nikamwangalia anacheka na nani? Sikupata jibu na mwisho aliondoka huku anageukageuka akicheka. Aliona nini? Alishangaa kuona watu wanakula kwa ulafi huku akiwa na njaa? Tangu hapo nawaangalia vichaa kwa makini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgodo visa hii ni sister post ya nyingine kule HM ngoja nitakutag uisome kwa undani
Mkulu nae ana kichaa chake, akicharuka hutoa kauli za hovyo hovyo mara Mwafwaa, mimi sikuleta njaa, sikuleta tetemeko n. K ndio ukichaa huo

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi wale vichaa ambao hupiga kelele mfano "wananiijia hao wamekuja na mafisi iiiii sitakii sitakiii"

Unalizungumziaje hili

_ where ever you are remember me_
Kuna kitu kinaitwa Hallucination, ambapo hupelekea sehemu za ubongo zinazohusika na interpretation ya taarifa mbalimbali kufanya 'false' interpretation ya images na taarifa zingine(illusion) !

Ni kama inavyomtokea mtu aliyetumia madawa ya kulevya kama bhang, miraa kujiona yuko Ulaya au anaona maji kwenye kidimbwi barabarani yeye anaona ni mto au bahari!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante mkuu kwa kunifungua sehemu ya ufahamu wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka mshana me mwenyewe huwa nawaonea huruma sana huwa nawaza tu wale wanaume wanaoweza kuwapa mimba vichaa inakuaje kuaje jaman mpaka uweze kulala na kichaa kweli unashindwa kumuonea huruma kutokana na hali yake we unawaza ngono tuuuu
 
Kaka mshana me mwenyewe huwa nawaonea huruma sana huwa nawaza tu wale wanaume wanaoweza kuwapa mimba vichaa inakuaje kuaje jaman mpaka uweze kulala na kichaa kweli unashindwa kumuonea huruma kutokana na hali yake we unawaza ngono tuuuu
Shunie utajiri hutafutwa kwa namna nyingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…