Vichaa katu hawaungani!

Vichaa katu hawaungani!

Librarian 105

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
356
Vichaa 100 wanaweza kulindwa na mlinzi mmoja tu mwenye silaha. Na mlinzi akawa na amani kabisa ya kutoundiwa uasi wowote. Hili funzo kwenye maisha yetu ya kifamilia na kijamii.

Familia inaweza kuwa na ukoo mkubwa usio na faida ila tu kipindi cha misiba na harusi ndo wanakaa pamoja kushirikiana pamoja kutatua matatizo ya msimu.

Na jamii inaweza kuishi kivyake vyake ikikabiliwa na matukio ya kisiasa na kiuchumi lakini ikawa ni yenye kukomalia umoja wa kijamii kupambana na matokeo ya kisiasa na kiuchumi yenye kuwafukarisha na kuharibu maadili yao. Na kusahau msemo wa wahenga, "kinga ni bora kuliko tiba".

Nafikiri nimefahamika, kuna hekima ya kujifunza pia katika maisha ya wale tunaowaona ni vichaa kwa macho yetu.
 
Back
Top Bottom