SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,841
- 1,843
Ukistaajabu ya Corona utayaona ya CCM.
Kurudi kwa Sumaye CCM na kupokelewa kwa mbwembwe wakati ambapo makatibu wakuu wawili wakiitwa kuhojiwa ni dhihaka na vichekesho vya hali ya juu.
Sumaye kwa kipindi cha takribani miaka minne ametumia majukwaa ya upinzani kuinanga, kuizodoa, na kuisema CCM waziwazi, amemkosoa na kumzodoa Mh. Rais kwa muda wote huo bila kupepesa macho.
Tofauti na ndugu Membe, Kinana na Makamba ambao walijaribu kukosoa wakiwa ndani ya chama tena wakiwa na lengo la kuboresha.
Sasa eti imeonekana SUMAYE ni shujaa anayerudi nyumbani na hawa makada wengine ni waovu kuliko Sumaye. Ujumbe gani unatolewa katika nadharia hii? Kwamba ukitaka kukikosoa chama na viongozi wake na ubaki salama basi ni bora ujitoe kwanza then watukane kila uwezavyo alafu rudi CCM, watakupokea kwa shangwe.
BASHIRU katika hili umechekesha sana kaka, nadhani Sumaye angepokelewa kimya kimya then aitwe kamati ya maadili kwanza ili kuhojiwa kwa kina kabla ya kumshangilia hadharani.
Najua unajua ila nakujuza hadharani ili ujue cha kufanya kwa makada watiifu wanaokosoa na makada vigeugeu wanaoingia na kutoka kama SUMAYE