SoC02 Vichocheo vya mabadiliko katika elimu, biashara/uchumi/ujasiriamali, afya, utawala bora na demokrasia, kilimo, sayansi na teknolojia

SoC02 Vichocheo vya mabadiliko katika elimu, biashara/uchumi/ujasiriamali, afya, utawala bora na demokrasia, kilimo, sayansi na teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

Shusta

New Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Habari kwa kila mmoja.

Andiko hili linachochea mabadiliko kwenye nyaja za elimu ,biashara/uchumi/ujasiriamali, afya, utawala bora, demokrasia, kilimo, sayansi na teknolojia.

ELIMU

Ili kuchochea mabadiliko katika maendeleo ya elimu bhaasi yafundishwe ambayo yanaendana kulingana na mazingira ya wale wanao fundishwa. Kama ni mtoto kutoka mkoa wa Kagera afundishwe kulima ndizi,miwa na kahawa. Kama ni mtoto wa mkoa wa Mwanza na Shinyanga wafundishwe kulima pamba. Mtaala uzingatie mazingira ya wanaojifunza na hiyo ni kwa nyanja zote kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu.

Mabadiliko kwa staili hiyo yanaweza kupatikana Kwa sababu watu watakuwa wanajifunza kutokana na mazingira na vitu wanavyoviona vilivyopo katika mazingira yao ili wakitoka wakaenda kwingine bhaasi hao watakuwa wazuri katika kuwafundisha wengine, kuliko wale wanaofundishia vitabu na uhalisia hauonekani.

BIASHARA, UCHUMI NA UJASIRIAMALI
Wataalamu wa uchumi wakihamasisha kutoa elimu ya kutosha kuhusu watu wanavyoweza kujiimalisha kiuchumi, na hasa katika kufanya biashara nakuleta mabadiliko ya kujua kama ni zao, bhaasi ni zao gani la kibiashara linaloweza kupata masoko, watu wapate manufaa na biashara wanayoifanya Kwa wafanya biashara wa viwanda na wafanya biashara wadogo wadogo.

Kuwe na mabadiliko ya viwanda,mabadiliko ya uzalishaji,mabadiliko ya usambazaji na kuwe na watu maalaumu wanaosimamia shughuli hiyo ili ifanyike Kwa manufaa ya wafanya biashara wote. Wafanya biashara wadogo wadogo (mf.wamachinga, mamantilie na kuendelea) hao wote wasimamiwe vizuli, Serikali iwasimamie hasa wizara ya viwanda na biashara wasimamie Kwa pamoja na wizara mama tamisemi na sio kuwanyanyasa kwakuwafukuza katika maeneo yao, Wawasimamie, wawashauri pia wawaelekeze.

Serikali iboreshe miundombinu katika usafirishaji, usambazaji na uzalishaji. Lakini pia serikali ijitahidi kusimamia uhulu wa wazalishaji, wasambazaji na watumiaji, Ili kila mmoja apate kilicho haki kwake na asipate hasara.Kwa namna hiyo uchumi kwa mtu mmoja mmoja utakuwa na uchumi serikalini utaongezeka.

AFYA

Wataalamu wetu wa afya na watafiti wa kubwa wajitahidi kufanya ufatiliaji kutumia zaidi mazao yapatikanayo katika mazingira yetu. Wafanye utafuti na viwanda vianzishwe kwaajili ya kuchakata madawa ambayo hayatakuwa na gharama kubwa ukilinganisha na yaliopo sasa. Ili watu hata wa hali ya chini wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu ya madawa yanayotoka nje ya nchi bhaasi waweze kupata huduma hiyo.Lakini pia kuhakikisha kwamba usambazaji wa madawa katika maeneo yote kuanzia ngazi za zahanati, vituo vya afya, hospitali na hospitali za lufaa pamoja na hospitali kuu waweze kupata madawa yakutosha. Vituo vinavyopokea madawa viwekwe kalibu kila wilaya ili dawa zipatikane kwa wakati.kila kijiji kiwe na zahanati, iwe na vifaa vyote vya afya na iwe na Wataalamu wa matibabu na Wataalamu wa madawa .Lakini pia elimu itolewe kuhusu afya ya mazingira kwa kila mwananchi.

UTAWALA BORA

ElImu yakutosha itolewe katika ngazi zote kuanzia ngazi za vitongoji mpaka ngazi za juu.Haki itendeke na isimamiwe vizuri Kwa watawala na watawaliwa .Sheria iweze kuwasimamia wale wanao nyimwa haki zao au wale wasiotekeleza wajibu wao Kwa pande zote mbili .Kama ni wanaoongoza wasimamie haki na wale wanaoongozwa wapate haki zao.

DEMOKRASIA
Huu ni mfumo wa vyama vingi,nahii inafahamika sana Kwa watu wenye elimu tu sasa ili kuleta mabadiliko elimu itolewe hasa vijijini juu ya demokrasia,lakini pia uchaguzi ufanyike Kwa uhulu na haki kupitia tume hulu .Iwepo sheria ambayo itawaadhibiti wale ambao hawatatenda haki wala kutimiza hadi wazo ahidi wakati wa uchaguzi .Pia iwekwe sheria yakuwalinda viongozi na familia zao kutoka Kwa wananchi waliopotoka na sera potofu.

KILIMO

Wizara ya kilimo Kwa kushirikiana na wizara zote zinazo hamasisha maendeleo ya wananchi kuhakikisha wanatilia mkazo maendeleo ya kilimo ili kuleta tija. Utafiti ufanyike wa kina ambao utaonyesha kwamba maeneo fulani ambayo mazao fulani yanaweza yakastawi vizuli bhaasi yasimamiwe vizuri na mazao hayo ndio yatiliwe mkazo zaidi katika maeneo hayo na mazao hayo yaweze kufikishwa katika maeneo ambayo mazao hayo hayastawi wala hayapatikani,

Kuliko ukulima wa holela holela bila utafiti wakutosha na kujilidhisha .Lakini pia watu wapewe elimu juu ya ifugaji bola wa mifugo (ng’ombe, mbuzi ,nguruwe, kuku nakadharika).Pia uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mborea ili ipatikane Kwa ulahisi na utafiti ufanyike kwamba mbolea hii inaweza kutumika wapi na kuzalisha wapi.Pia mahabara zijengwe kwaajili yakuchunguza vitu mbali mbali hasa katika mazao ambayo yanatumika kila siku.

SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Serikali ihakikishe maeneo maalumu yanayotoa elimu kuhusu sayansi na teknolojia wanapelekwa watu wakutosha kwa maana ya wanafunzi wapate elimu hiyo. (Mf.Wataalamu wa Tehama).Na elimu hii ingefaa kama ingetolewa kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu. Elimu hii ikielezwa kwa weledi nakutoa mafunzo yakutosha kwa wananchi na wanafunzi itaweza kusaidia katika sekta zote kwasababu mfumo wa kompyuta unalahisiha nakusaidia watu katika kufanya mambo Kwa wepesi zaidi kuliko mfumo wa kizamani.

Mf.Posta wanasafirisha mfumo wa maandishi yale yaliyo andikwa Kwa mkono au yale yaliyochapwa yakafungwa pamoja, lakini ukitumia kompyuta unatuma Kwa njia ya barua pepe ambayo hulahisisha zaidi. Mf. Uwagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi mtu anaweza kutumia mfumo huo huo wa sayansi na teknolojia kuagiza bidhaa mfumo usio hitaji kusafiri badala yake unasafiri Kwa taalifa kupitia kwenye mtandao.Serikali inabidi isimamie wamiliki wa mitandao ili kuhakikisha kila mwananchi anafaidika kutokana na matumizi yake binafsi.Pia wizara ya sanaa na michezo ikishilikiana na wizara ya tamisemi wazingatie maadili na tamaduni zetu za kiafrika nikimaanisha kupiga malufuku Kwa matumizi mabaya ya mitandao kama kutuma picha za uchi katika mitandao ya kijamii jambo hilo inabidi litiliwe mkazo zaidi ili utamaduni wetu uzidi kudumishwa.

Nina Malizia kwa kusema kwamba Sayansi na teknolojia ikisimamiwa vizuli kila kitu kitakuwa sawa kuanzia sekta ya elimu, biashara/uchumi/ujasiriamali, afya, utawala bora, demokrasia na kilimo.

ASANTENI.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom