SoC01 Vichocheo vya ukuaji wa Uchumi wa Tanzania yetu

SoC01 Vichocheo vya ukuaji wa Uchumi wa Tanzania yetu

Stories of Change - 2021 Competition

KIKOTI12

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
3
Reaction score
0
Uchumi hupimwa kwa ongezeko la Pato la ndani la nchi ambalo nchi inakuwa umepata kwa mwaka mmoja. Kuna sababu nyingi zinazopelekea ongezeko Hilo. Kwenye nchi nyingi hupimwa pia kwa jinsi gani watumiaji wa bidhaa wananunua na uwekezaji wa bidhaa. Kama mtumiaji anauwezo wa kununua mahitaji yake kwa urahisi, kuongezeka kwa mishahara na wawekezaji kukuza kazi zao. Kuongezeka kwa teknolojia na matumizi.

Uchumi hautegemeani na sababu moja ambayo inaweza fanya unaendelea, sababu zipo nyingi sana, Vitu tunavyo weza kuzingatia ili tuweze kuendelea kiuchumi

1. Kupunguza mzigo wa Kodi

Wafanyabiashara kurahisishiwa kwa kupunguziwa malimbikizo ya Kodi. Ambalo punguzo Hilo litamsaidia mfanyabiashara kukuza biashara yake. Kuwa na mtaji mwingi, kuboresha teknolojia, vitendo hivyo vyote vinaongeza uzarishaji.

2. Kupunguza Sheria kandamizi zinazobana uchumi

Kuondoa Sheria kandamizi zinazo bana shughuli mbali mbali za uchumi Kama viwanda na biashara. Sheria nyingi zimekuwa zikiwabana wakuza uchumi kufanya kazi zao na serikali kutokuwa na maono kwa wananchi wake. Serikali kutokuwa na maono Inapelekea vikwazo kwa uchumi.

3. Kuwa na matumizi mazuri ya miundombinu kukuza uchumi

Kukua kwa miundombinu hutokana na pale serikali inapotumia fedha kwa kuendeleza na kujenga miundombinu, ambayo ni kichocheo Cha uchumi ambapo shughuli zote za uchumi zinakuwa zinafanyika kwa usahihi. Vyombo vya kusafirisha mizigo kama magari. Kama ikitokea miundombinu haipo sawa inasababisha mrundikano wa magari barabarani ambapo itafanya uchumi kukwama kuendeleza.

4. Kuwa na uwekezaji mkubwa katika Elimu/Serikali na wadau mbalimbali kutulia mkazo Elimu

Njia moja wapo ya kuwa na uchmi imara ni pamoja na nchi kuwa na elimu yenye ubora. Wadau na serikali itoe nafasi na kipaumbele cha ufadhili wa elimu njee ya nchi mbalimbali na ndani ya nchi ili kuwa na watu wenye uzoefu tofauti. Kwa kufanya hvyo nchi inakuwa na msingi mzuri wa kukuza uchumi wake. Nchi zote ambazo uchumi wake upo imara wamefanya uwekezaji mkubwa katika elimu.

5. Kulipa Kodi

Wananchi tunatakiwa tuwe kichocheo kwa kulipa Kodi kwasababu Kodi hizo ndio zinazoenda kuweka sawa miundombinu na kuboresha mifumo mizuri ya Elimu. Kodi zina mchango mkubwa sana maana nchi bila ulipaji mzuri wa Kodi hatuwezi kuwa na uchumi imara.

6. Kutilia mkazo katika ujasiriamali

Watu wanatakiwa wapewe motisha ya kufanya ujasiriamali kwa kutengenezewa masoko mazuri, kuwekewa utaratibu mzuri wa kufanya kazi zao, kutosumbuliwa na migambo wa jiji na manisipaa. Wajasiriamali Wana sehemu kubwa sana katika mzunguko biashara na ukuaaji wa wa uchumi

7. Kutolewa kwa mikopo yenye masheriti nafuu

Mfano kwa watu Kama wasomi ambao wamemaliza vyuo na wanasubiri ajira. Hii no nafasi yao kwa kupewa mikopo yenye mazingira nafuu kwa ajiri ya kuvutia ukuaji wa uchumi. Wapewe mikopo wafanye miradi tofauti tofauti ili kukuza uchumi tofauti na kukaa tu bila kazi za kufanya ambapo linakuwa janga kwa taifa.

8. Kuruhusiwa kwa biashara ya forex na hela za kidigitali

Fedha hizi zina nafasi yake, kwani watu wa nchi zinazoendelea na zilizo endelea wanafanya forex na uzungushaji wa biashara kubwa Kama mfano hivi kalibuni tunaona watu Kama Elon musk na Tesla wamefanya uwekezaji mkubwa sana wa Bitcoin Kwenye biashara ambazo kwa Tanzania hicho kitu ni kigumu.

Hitimisho

Serikali na viongozi wetu wanatakiwa wawe na maono, na malengo juu ya taifa letu, wakiwa kwenye vikao vya wizara na bunge wapitishe Sheria ambazo zitavutia uwekezaji katika nchi yetu. Wawekezaji wengi wanashindwa kuwekeza Tanzania kwasababu ya Sheria kandamizi. Hivyo vyote vinakuwa vikwazo vya maendeleo ya uchumi kwani wawekezaji Wana sehemu yao katika uchumi.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom