Vichwa Vipya 3 vya Treni ya Umeme SGR Vyawasili Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

TRC YAPOKEA VICHWA 3 VYA TRENI YA UMEME SGR KUTOKA KOREA KUSINI

Shirika la Reli Tanzania limepokea vichwa vipya vitatu (3) vya treni za umeme vilivyoundwa na kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya abiria yaliyoundwa na kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) kutoka nchini Korea Kusini.

Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria kwa ajili ya undeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR.

Mpaka sasa Shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne (4) kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) ya nchini Korea Kusini.

Mabehewa matatu (3) yaliyosalia yanatarajiwa kuwasili chini Februari, 2024. Vichwa 13 vilivyobaki vinatarajiwa kuwasili kwa awamu kama ifuatavyo, vichwa sita (6) vitawasili mwezi Machi na vichwa saba (7) vitawasili Aprili, 2024.

 

Attachments

  • GCp3m0xWwAAgrZa.jpg
    336 KB · Views: 9
  • GCp3m0qWcAAqbl5.jpg
    310.4 KB · Views: 8
Bora mmalizie kwanza kujenga reli kuliko kuviweka tu hapo viliwe na kutu mwisho quality assurers waje waseme havifai tena
 
Hiyo ni treni ya 1935 kabla ya hitler kutaka kutawala dunia...uongozi wote ccm umejaa majambazi hii ni aibu ya karne,mama apumzike ampe kijiti abdul
 
Alishindwa kuagiza mabasi mapya ya mwendo kasi ndio walete vipya vya treni?

Hakuna kitu kama hicho.

Vichwa ni vipya mkuu, unless uwe umeamua tu kutokuamini...

BRT ni mradi wa serikali lakini mwenye mabasi sio serikali hata hivyo mabasi ya BRT huletwa mapya kabisa sio mtumba...
 
Mabehewa kama yale yanatumika sehem nyingi tu.
Pia yale ni kama vile mabehewa ya economy kuna mabehewa ya first na second class utayaona.
Na kumbuka treni yetu ni elektric lokomotiv sio EMU .
 
Mabehewa kama yale yanatumika sehem nyingi tu.
Pia yale ni kama vile mabehewa ya economy kuna mabehewa ya first na second class utayaona.
Na kumbuka treni yetu ni elektric lokomotiv sio EMU .
Nilichojifunza watu wengi hawajajua bado utofauti wa EMU na loco hauled trains. Ni kweli kabisa hayo mabehewa yanatumika kwingi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…