Vichwa vya treni ya SGR kupewa jina la "Samia Express", Watanzania tumekwama wapi?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Naishukuru Serikali kwa kupitia Shirika la reli Tanzania TRC kwa kuendelea na jitihada za kuboresha miundombinu yetu la reli.

Ila kinachonisitikisha, ni uamuzi wa kupachika jina la Mwenyekiti wa chama cha Siasa(CCM) bla kuwashirikisha Wananchi Wanaotoa kodi zao. Hii ni haki kweli?


Naamini Watanzania tuna uwezo mkubwa wa kufikiri zaidi ya huu.

Je, Dr. Samia kawalazimisha au ni Kada mmoja yupo huko TRC kaamua kujipendekeza?

Je, kama nchi tunaelekea wapi? Ni wapi tumejikwaa? Hii ni moja ya matumizi mabaya ya madaraka. Tunapoenda Wahuni watakuwa wanajifungia ndani asubuhi wanakuja wameadilisha jina la mbuga ya Ngorongoro.

Kutoka maktaba Raia wa Nachingwea kwa Mara ya kwanza wamaipokea Treni ya kutoka mkwaya hadi Nachingwea
Oktoba 25, 1949

Mao-Tse-Tung wa China akiwa na Julius K. Nyerere alipoenda kuwaomba Wachina wamalizie mradi wa reli ya TAZARA. 01 Jan 1960.

Mungu azidi kutuongoza na kuwasimia Viongozi waliopo Madarakini Watufikirie Sisi Wananchi kabla ya kujiangalia wao
 
Nipeni kura zenu hadi jina la nyerere nitalifuta kila sehemu
 
Hilo lina madhara gani katika uchumi wetu, au kwa ufanisi wa hilo shirika, sometime chuki ni mbaya huyu ni Raisi wa nchi hi.......
 
Lakini stendi ilivopewa magufuli bus terminal mbona mlishangilia sana
 
"Kizuri chajiuza, KIBAYA chajitembeza"

Mleta mada wala usijitaabishe kwa Mambo kama haya ya watu walioshindwa....wanazidi kujiweka wazi kwamba wamefilisika na hawana la ziada la kuwapa/fanyia wananchi.
Inabidi wajitangaze ili wajulikane kwamba wapo, maana hata wao wenyewe wanajua kwamba wamesahaulika kwa wananchi.

Ukiona mtu anaparamia mpaka kodi ya mwanachi inayotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na anasema ni pesa yake, basi ujue ni debe tupu.
 
Huyu mama ipo siku atataka Tanzania iitwe Samia Suluhu!!

Ni kama ana shida kubwa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…