Vicky Kamata afunguka kuhusu ndoa yake

Vicky Kamata afunguka kuhusu ndoa yake

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa kubainika kuwa mwanaume aliyetaka kufunga naye ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni habari za kutungwa.

Vicky Kamata ameiambia amplifaya ya Clouds fm jana kuwa maneno mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofunga yalikuwa yametengenezwa na watu.

"Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja na hayo mimi bado nasema mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa ajaruhusu kuwa tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa.

Mimi kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga vinginevyo, kwaiyo siku zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo mapenzi ya binadamu.

Ni kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka 2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo bila kuwa nimemchunguza huyo mtu.

Kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke wake , mke wake alikwenda kuzuia Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest zao.

Lakini siyo kwamba nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu ata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu, aliongea na vyombo vya habari akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi.

Kwaiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke wake amezuia yalikuwa ni maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo kweli.

Kuhusu kwamba ajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi nafahamu kwamba yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama ambavyo
mimi naendelea na shughuli zangu kama kawaida.

Tunawasiliana, yani cha kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi, hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini mungu ndo mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo.

Kwaiyo kama Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na binadamu mwingine hataki bado ingefungwa, kwaiyo mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge wenzangu wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe.

Mimi ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyo"Alisema Vicky
 
Pole mchumba kaogopa kubabusewaaaa
 
Pole mwaya najua inauma, ila acha uwongo haiwezekani ndoa ikaachwa kufunga bila sababu ya msingi; eti kuumwa no way. Wakati mwingine tunmsingizia Mungu eti mapenzi ya Mungu! Umesema "aliyekuwa mchumba wangu' kwa hiyo sasa hivi sio mchumba tena? Kitu gani kimesababisha useme "aliyekuwa mchumba wangu" usiseme " mchumba wangu" embu funguka mama.
 
Ila haujaelezea sababu rasmi ya kuhairishwa ni huo ugonjwa wako wa ghafla ama???
 
haoni hata ibu; speak out kuwa uliingizwa mjini, utaeleweka kurukaruka kama hivi ndio kunasababisha kila mtu aseme kivyake
 
Pole sana Vicky..kwasababu ndoa ilihairishwa kwa sababu ya ugonjwa na sasa umeshapona..je ndoa inafungwa lin tena????au ndio haipo tenaaaa?????
 
Ningekuwa mimi nisingeongea Ngo"do! unavyoongea ndivyo unavyozidi kuwapa watu maswali na kuendelea kusema wenyewe tulishasahau , tupo kwa Komba sasa unaturudisha nyuma lol!Mwanamke Tulia
 
Pole sana Vicky..kwasababu ndoa ilihairishwa kwa sababu ya ugonjwa na sasa umeshapona..je ndoa inafungwa lin tena????au ndio haipo tenaaaa?????

swali zito sana hili, ngoja yangu niyaweke kiporo tusije tukamchanganya bure.
 
Pole Vicky, kwa yote binadamu wengi tuna historia mbaya kwa namna moja au nyingine ktk maisha yetu, na baadaye huwa zinakuja kutuhukumu. Lakini unapaswa kujutia na kurekebisha na maisha yakasonga mbele. .
Mi naona ungenyamaza maana sababu unayosema ya kuugua na si ugonjwa mahututi hauwezi kufanya ndoa kuhairishwa au kutokufungwa kabisa, maana wanawake wanavyopenda kuvaa shela eti ahairishe kisa anaumwa!!! ukweli mnaujua nyinyi wenyewe we nyamaza .
 
Acha porojo vicky lini sasa itafungwa hiyo ndoa? Nini chanzo cha kutofungwa hiyo may?
 
Back
Top Bottom