Vicoba na michezo ya kupeana hela vinaweza kusababisha changamoto ya afya ya akili kwa wanawake

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 48:
Nakiri kwamba Vicoba na michezo ya kutoana/kupeana hela vinawasaidia wanawake kujikimu mahitaji yao madogo madogo ya nyumbani.

Hata hivyo kumeibuka wimbi la wanawake wengi kujiunga kwenye vicoba vingi na idadi kubwa ya vikundi vya kutoana/kupeana hela kuzidi uwezo wao wa kifedha.

Mzigo wa marejesho ukiwaelemea wanawatwisha waume/wapenzi wao mizigo hiyo, na mambo yanapokwenda "ndivyo sivyo" wanatumbukia kwenye malumbano ya ndoa na msongo wa mawazo.

Baadhi ya wanandoa wametengana kwasababu ya ugomvi uliosababishwa na marejesho ya Vicoba.

Mwanamke anapoona mumewe ameshindwa kumsaidia marejesho anaamua kuchepuka ili apate pesa za marejesho, au makasiriko ya mara kwa mara.

Kuna familia nyingine zimelazimika kuuza mali zao ili kulipa madeni (marejesho) ya vicoba.

✍️Vicoba na michezo ya kupeana hela vinaweza kusababisha changamoto ya afya ya akili kwa wanawake.​

Right Marker
Dar es salaam
 
Vicoba na kupeana fedha wanaocheza wanawake huvuruga ndoa sana. Mke atataka apate hela za michezo hiyo kila mara. Sasa kama msela huna hela ya kumpa mkeo ni dhahiri kuna dokozi litampa mkeo hela akacheze mchezo huo kwa malipo ya kutoa uroda
 
Mhadhara - 48:
Nakiri kwamba Vicoba na michezo ya kutoana/kupeana hela vinawasaidia wanawake kujikimu mahitaji yao madogo madogo ya nyumbani.

Hata hivyo kumeibuka wimbi la wanawake wengi kujiunga kwenye vicoba vingi na idadi kubwa ya vikundi vya kutoana/kupeana hela kuzidi uwezo wao wa kifedha.

Mzigo wa marejesho ukiwaelemea wanawatwisha waume/wapenzi wao mizigo hiyo, na mambo yanapokwenda "ndivyo sivyo" wanatumbukia kwenye malumbano ya ndoa na msongo wa mawazo.

Baadhi ya wanandoa wametengana kwasababu ya ugomvi uliosababishwa na marejesho ya Vicoba.

Mwanamke anapoona mumewe ameshindwa kumsaidia marejesho anaamua kuchepuka ili apate pesa za marejesho, au makasiriko ya mara kwa mara.

Kuna familia nyingine zimelazimika kuuza mali zao ili kulipa madeni (marejesho) ya vicoba.

✍️Vicoba na michezo ya kupeana hela vinaweza kusababisha changamoto ya afya ya akili kwa wanawake.​

Right Marker
Dar es salaam
Kuna familia mahusiano yamevunjika,ndoa zimevunjika,wameu
uwana,wengine wamekufa kwa kujinyong au kunywa sumu,wengine wameishia kupata magonjwa ya pressure,visukari,kufukuzwa kazi n.k....
 
Back
Top Bottom