BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Mfumo wa VICOBA au Saving group ni mfumo ulio asisiwa nchini Inida miaka ya 80 mwishoni na kwa bara la Africa mfumo huo ilingia miaka ya 90 na kuanzia kule Niger.
Mfumo Wa VICOBA una madhumuni makuu matatu;
Wengi humu ni mashahidi wa vikundi vya VICOBA mitaani huko, wapo kweli walio fanikiwa ila ni kwa asilimia ndogo sana na asilimia kubwa ni matatizo, kuna hadi ndoa zimevunjika, kuna ugomvi umetokea kuna watu wameuizwa mali kwa sababu ya VICOBA.
Kwanini VICOBA vimeshindwa mtaani?
Hakuna Upendo miongoni mwa wana vikundi, hii ni moja ya nguzo kuu ya VICOBA, watu wengi ni wanachukiana hata ndani ya vikundi.
Elimu ya kifedha ilipaswa kuanza kabla ya VICOBA na watu kwa sababu ni watu wazima tiyali ikawa ngumu.
Wanachama baadhi huingia wakiwa na malengo ovu.
Kikundi kuwa na watu wa matabaka tofauti, hii ni kosa kubwa sana,
Wanachama kukosa elimu ya kifedha tangu awali kumepelekea haya yote, watu kukopa na kwenda kufanyia vitu visivyo na tija kama vile; Harusi, kununua nguo, kuhonga, Kununua vitu kama simu.
VICOBA/Saving group Kwa watoto wadogo
Wazo la kuwaanzishia vikundi vya kuweka akiba na kukopa VICOBA kwa watoto wadogo wa umuri wa miaka 5 hadi 12 au 15 ni wazo zuri sana na jema. Watoto wadogo wanaweza leta matokeo chanja kwenye jamii ukilinganisha na watu wazima hasa kwa baadae.
Kwanini Watoto wadogo?
Wana upendo sana miongoni mwao,
Hawatakuwa na Malengo ovu zaidi ya lile lengo kuu la kuweka akiba na kukopa.
Watakuwa sawa viwango sawa kwa umri na kwa kila kitu
Itawajenga sana kutengeneza confidence ya kutosha itakayo wasaidia mbeleni.
Elimu ya kuweka na kukopa itawaingia sawa sawa kwa sababu ni wadogo.
Watoto wadogo waatakapo anza kukua na mfumo wa kujiwekea akiba na kukopa watakuwa wakijua jinsi ya kuja kukopa kwenye taasisi kubwa za kifedha kuliko ilivyo sasa ambapo hata watu wazima asilimia kubwa hatuna elimu zakifedha na ndo maana tunajinunulia tu vitu hovyo hovyo na pia tunakopa na kurejesha inakuwa taabu sana.
Huu mfumo utafanya kazi kwa njia kuu mbili;
Kuwapa pesa ya kwenda kununua hisa
Kusimamia mikopo watakayo kopa
Kuwaruhusu watoto kwenda kwenyekikundi
Kuwa sehemu ya mtoto na siku zingine kwenda kwenye kikundi kuona wanavyo endesha kikundi.
Mfumo unaweza kufanya vipi kazi?
Mfumo utafanya kazi kwa wazazi mtaani kujiunga na kuhamasisha kikundi cha watoto wao, inaweza ikawa ni wale marafiki mnao fanya nao kazi, ndugu na kadhalika, ila mazingira ya watoto kukutana yawe rafiki sana kwao.
Watoto wawe ni wa hapo jirani wanapokaa /mtaa mmoja na wawe na umuri ambao hujaachana sana.
Watoto watapewa elimu kwanza ya umuhimu wa wao kuanza kujiwekea kabisa na kwa nini wanapaswa kuanza sasa kujifunza kujiwekea kabisa.
Zoezi laweza kuwa linafanyika kila weekend.
Wazazi wa watoto wanaweza kuwa wana hudhuria kama watazamaji tu na watakaa pembeni.
Kama watoto wako Boarding mfumo pia utafanya kazi chini ya usimamizi wa walezi wa watoto shuleni na kwa makubaliano ya wazazi ambao lazima wawe wanapata report.
KUNUNUA HISA
Katika mfumo kama huu wa VICOBA kwa watoto wadogo, watoto watakuwa wana nunua hisa zao au share kila siku wanayo kutana na kila mtoto atanunua kulingana na atakavyo kuwa amepewa pesa na mzazi wake na kwa sababu walisha pewa elimu mwanzo watakuwa wanajua kila kitu kinacho endelea.
KUKOPA
Watoto watakuwa wanakopa kama sehemu yao ya kujifunza na sio kama kwenda kutatua matatizo kwenye familia zao, mtoto anaweza propose kwa wazazi wake kwamba anataka kukupa pesa kwenye kikundi kwa ajili ya mambo Fulani, na hapa sasa wazazi watampima mtoto kiwango chake cha elimu ya kifedha, Mtoto atataja vitu anavyo taka kununua kwa mfano: Kununua nguo, Kununua toy, kwenda kutembea, kununua Baiskel, vitabu,kununua Computer na kadhalika.
Watoto wa takuwa wanajieleza mbele za watoto wenzao kwamba wanakopa kufanyia nini na hapo watoto watakuwa wana fanya majadiliano na hapa ndio sehemu muhumu ya wazazi kuwepo kusikiliza na kutoa maoni ikibidi.
RIBA
Wazazi watasaidia kuwapangia riba, ingawa pia hapa kwa sababu ni mafunzo haitakuwa ile riba ya kuwakamua bali ni riba ya wao kujifunza.
MWISHO WA MWAKA
Kwa sababu vinaenda kwa cycle mwisho wa mwaka wanakuwa wanagawana pesa na hapa ndio pia sehemu ya wewe mzazi kupanga na motto wako kwamba hii fedha mnaifanyia nini.
Faida za VICOBA kwa watoto wadogo
Watoto wadogo kipindi wanakuwa ndio kipindi wana install mambo kwenye ubongo wao, hivyo kuinstall elimu ya kuweka akiba na kukopa ni jambo la kipekee kabisa kwenye maisha yao ya baade.
Huu mfumo ni wa kutoa elimu ya kutunza fedha na kukopa , na mtoto anapo kuwa mkubwa sasa hana haja tena nahuu mfumo wa vikundi bali anaweza sasa hata kudili na taasisi rasimi za kifedha kama Mabenki.
Binafisi naandaa mwongozo ya VICOBA kwa ajili ya watoto na siku itakapo kuwa tiyali nitakuja kushare na wadau humu.
Taifa na jamii kwa ujumla tunaweza tengeneza kizazi bora sana kwa baadae.

- Kuwapa furusa wale walio tengwa na huduma rasimi za kifedha(Financial exclusion)
- Kuwandaa watu kwenda kukopa au kupata huduma kwenye taasisi rasimi kama Mabenki
- Kutoa elimu ya kifedha(Financia literacy) kwa wanachama au wana kikundi.
Wengi humu ni mashahidi wa vikundi vya VICOBA mitaani huko, wapo kweli walio fanikiwa ila ni kwa asilimia ndogo sana na asilimia kubwa ni matatizo, kuna hadi ndoa zimevunjika, kuna ugomvi umetokea kuna watu wameuizwa mali kwa sababu ya VICOBA.
Kwanini VICOBA vimeshindwa mtaani?
Hakuna Upendo miongoni mwa wana vikundi, hii ni moja ya nguzo kuu ya VICOBA, watu wengi ni wanachukiana hata ndani ya vikundi.
Elimu ya kifedha ilipaswa kuanza kabla ya VICOBA na watu kwa sababu ni watu wazima tiyali ikawa ngumu.
Wanachama baadhi huingia wakiwa na malengo ovu.
Kikundi kuwa na watu wa matabaka tofauti, hii ni kosa kubwa sana,
Wanachama kukosa elimu ya kifedha tangu awali kumepelekea haya yote, watu kukopa na kwenda kufanyia vitu visivyo na tija kama vile; Harusi, kununua nguo, kuhonga, Kununua vitu kama simu.
VICOBA/Saving group Kwa watoto wadogo
Wazo la kuwaanzishia vikundi vya kuweka akiba na kukopa VICOBA kwa watoto wadogo wa umuri wa miaka 5 hadi 12 au 15 ni wazo zuri sana na jema. Watoto wadogo wanaweza leta matokeo chanja kwenye jamii ukilinganisha na watu wazima hasa kwa baadae.
Kwanini Watoto wadogo?
Wana upendo sana miongoni mwao,
Hawatakuwa na Malengo ovu zaidi ya lile lengo kuu la kuweka akiba na kukopa.
Watakuwa sawa viwango sawa kwa umri na kwa kila kitu
Itawajenga sana kutengeneza confidence ya kutosha itakayo wasaidia mbeleni.
Elimu ya kuweka na kukopa itawaingia sawa sawa kwa sababu ni wadogo.
Watoto wadogo waatakapo anza kukua na mfumo wa kujiwekea akiba na kukopa watakuwa wakijua jinsi ya kuja kukopa kwenye taasisi kubwa za kifedha kuliko ilivyo sasa ambapo hata watu wazima asilimia kubwa hatuna elimu zakifedha na ndo maana tunajinunulia tu vitu hovyo hovyo na pia tunakopa na kurejesha inakuwa taabu sana.
Huu mfumo utafanya kazi kwa njia kuu mbili;
- Mtaani, yaani wanakoishi hawa watoto na wazazo wao
- Shuleni - endapo wapo Bording; na Vyuoni.
Kuwapa pesa ya kwenda kununua hisa
Kusimamia mikopo watakayo kopa
Kuwaruhusu watoto kwenda kwenyekikundi
Kuwa sehemu ya mtoto na siku zingine kwenda kwenye kikundi kuona wanavyo endesha kikundi.
Mfumo unaweza kufanya vipi kazi?
Mfumo utafanya kazi kwa wazazi mtaani kujiunga na kuhamasisha kikundi cha watoto wao, inaweza ikawa ni wale marafiki mnao fanya nao kazi, ndugu na kadhalika, ila mazingira ya watoto kukutana yawe rafiki sana kwao.
Watoto wawe ni wa hapo jirani wanapokaa /mtaa mmoja na wawe na umuri ambao hujaachana sana.
Watoto watapewa elimu kwanza ya umuhimu wa wao kuanza kujiwekea kabisa na kwa nini wanapaswa kuanza sasa kujifunza kujiwekea kabisa.
Zoezi laweza kuwa linafanyika kila weekend.
Wazazi wa watoto wanaweza kuwa wana hudhuria kama watazamaji tu na watakaa pembeni.
Kama watoto wako Boarding mfumo pia utafanya kazi chini ya usimamizi wa walezi wa watoto shuleni na kwa makubaliano ya wazazi ambao lazima wawe wanapata report.
KUNUNUA HISA
Katika mfumo kama huu wa VICOBA kwa watoto wadogo, watoto watakuwa wana nunua hisa zao au share kila siku wanayo kutana na kila mtoto atanunua kulingana na atakavyo kuwa amepewa pesa na mzazi wake na kwa sababu walisha pewa elimu mwanzo watakuwa wanajua kila kitu kinacho endelea.
KUKOPA
Watoto watakuwa wanakopa kama sehemu yao ya kujifunza na sio kama kwenda kutatua matatizo kwenye familia zao, mtoto anaweza propose kwa wazazi wake kwamba anataka kukupa pesa kwenye kikundi kwa ajili ya mambo Fulani, na hapa sasa wazazi watampima mtoto kiwango chake cha elimu ya kifedha, Mtoto atataja vitu anavyo taka kununua kwa mfano: Kununua nguo, Kununua toy, kwenda kutembea, kununua Baiskel, vitabu,kununua Computer na kadhalika.
Watoto wa takuwa wanajieleza mbele za watoto wenzao kwamba wanakopa kufanyia nini na hapo watoto watakuwa wana fanya majadiliano na hapa ndio sehemu muhumu ya wazazi kuwepo kusikiliza na kutoa maoni ikibidi.
RIBA
Wazazi watasaidia kuwapangia riba, ingawa pia hapa kwa sababu ni mafunzo haitakuwa ile riba ya kuwakamua bali ni riba ya wao kujifunza.
MWISHO WA MWAKA
Kwa sababu vinaenda kwa cycle mwisho wa mwaka wanakuwa wanagawana pesa na hapa ndio pia sehemu ya wewe mzazi kupanga na motto wako kwamba hii fedha mnaifanyia nini.
Faida za VICOBA kwa watoto wadogo
Watoto wadogo kipindi wanakuwa ndio kipindi wana install mambo kwenye ubongo wao, hivyo kuinstall elimu ya kuweka akiba na kukopa ni jambo la kipekee kabisa kwenye maisha yao ya baade.
- Watoto wanakuja kuwa na uelewa mkubwa sana wa elimu ya kifedha.
- Inawajengea confidence.
- Itasaidia kuwanaadaa watoto kwa maisha ya baadae.
- Ni elimu nzuri sana nje ya mfumo wa elimu ya Darasani,
- Mtoto/Watoto wanaweza kuja kuwa wasimamizi bora kabisa wa mali au project za wazazi wao.
- Mtoto atakuwa na uchungu sana na kile kitu alicho nunua kwa pesa ya mkopo kwa sababu atajua fika ile pesa inarudiswa na endapo motto aliko[a kuongezea ada ya shule basi motto atakuwa makini sana shuleni kwa kujua ile pesa inapaswa kurudishwa.

Upvote
3