Nkaburu
JF-Expert Member
- Mar 23, 2023
- 1,638
- 1,961
Somalia imemsimamisha kazi afisa wa ngazi ya juu wa riadha baada ya mmoja wa wanariadha wake kuweka rekodi mpya ya mbio za mita 100 - ambayo ni ya polepole zaidi kuwahi kutokea katika mashindano ya kimataifa.
Mwanariadha huyo Nasra Ali Abukar, alikimbia na alivuka mstari wa kumaliza kwa sekunde 21.81, karibu sekunde 10 nyuma ya mshindi.
Source: Aljazeera.com
=====
Wizara ya Michezo ya Somalia imemfuta kazi Bi. Khadija Aden (pichani chini) ambaye ni bosi wa Shirikisho la Riadha nchini humo baada ya kubaini kuwa Nasra Abukar Ali (20), ambaye aliiwakilisha nchi kwenye mashindano ya FISUGames nchini China hakuwa mwanariadha wa kulipwa wala mwanafunzi wa chuo kikuu.
Nasra ambaye alipewa nafasi kwa kuwa ni ndugu wa bosi huyo, alimaliza mbio za mita 100 kwa sekunde 21, huku mitandaoni nchini china akitajwa kuwa ni “mwanariadha mbovu zaidi” katika mashindano hayo.