Video: Duh Wabongo mnalo.... hili la vyeti lifanyike Kenya pia

Video: Duh Wabongo mnalo.... hili la vyeti lifanyike Kenya pia

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Wengi mna vyeti bandia na kushikilia nyadhifa muhimu, mnatuzingua sana huku JF, ving'ang'anizi balaa, unakuta mtu hata umueleweshe vipi, kashikilia ule msimamo na habadiliki na baada ya miezi kadhaa bado anaibuka na ile ile mada kama ameshikilia huo msimamo wa mwanzo.

Mnafuatwa na polisi hadi maofisini huko huko mlipo, JF itapungua v.ilaza.
Naomba hii ije Kenya pia, sio kosa kuiga mazuri.


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watatu wakazi wa buguruni kwa kosa la kukutwa na nyaraka bandia za serikali kama vyeti vya kidato cha nne, stika za SUMATRA, vyeti vya vyuo vya uuguzi, vyeti vya kuzaliwa, leseni bandia za biashara, nyaraka za bima pia walikutwa na mihuri mbalimbali ya ofisi za serikali na binafsi.

Watuhumiwa wote bado wapo rumande na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani, baada ya mahojiano na polisi watuhumiw hao wamekiri kuuza vyeti watu wengi ambao wako kwenye ajira.

Akizungumza na waandishi wa habari kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema……….>>>’Wanataja na wanaendelea kutaja watu ambao wamewauzia vyeti na wameshapata ajira serikalini, kama ulinunua hiki cheti, nataka niseme ni balaa kwako kwa sababu watatutajia kila mmoja mmoja na tutakufuata huko ulipo’.

>>>’Hatuishi hizi nyaraka tulizozipata tutakwenda mbali zaidi kwa kuwanyofoa mmoja mmoja aliyejipatia kazi kwa kutumia hivi vyeti bandia’

VIDEO: Polisi wana mpango huu kwa wale wenye vyeti feki maofisini - millardayo.com
 
Hii ishu inafika mbali sana, ambapo macho na fikra zangu haziwezi fika.
So deeply rooted in our society.
HAPA KAZI TU!
 
Kwa msako huu kama kuna mtumishi mwenye cheti fake nje ya majeshi atanusurika basi hakuna tufani lingine la vyeti litakalomtikisa.
 
Hii ingeanzia ndani ya majeshi yetu ingekuwa poa sana , naomba hii kasi isishuke iendelee mpaka heshima irudi
 
Lazima na wao waishi km mashetani sema hao jamaa walikuwa watundu mnooo
 
Huko tunaweza kubakiza askari 50 tu. Hii vita ni ngumu maana hata kwenye baraza la mawaziri wamo pia. Huwa najiuliza Mwigulu ni jina la kisukuma lakini mbona linapatikana Iramba?
Kuna mwingine jina lake ni Andrea mkuu.
 
tumbua tuuu magu.. vijana wengi wapo kitaa, mijitu ikalia ajira zao na kujinafas..
 
ndg. yang mk254, hawa watu wa vyeti feki wanarudisha sana gurudumu la maendeleo, ufanisi ktk kazi umekuwa ukipungua kwa sababu ya hawa watu. wanatakiwa kusakwa popote walipo,

Hehehe Kwa hili nakubaliana na wewe 100%
Mijitu ipo ofisini imevaa suti na tai lakini ukiingia nao vikao, unashangaa walifika hapo vipi kwa jinsi wanavyoboronga.
 
Back
Top Bottom