Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo nikapanda bolt kutoka airport, kabla hatujaanza safari dereva akaingia kituo cha mafuta cha O-Lake airport, wakati wa kutoka naona traffic anaongoza magari na mengine anayakataa kukunja, kumbe anaongoza magari yanayoenda kujaza gesi kituo kwasababu yana kawaida ya kuziba barabara ya Mwl. Nyerere kutokana na urefu wa foleni.
Nimekadiria kwa google earth kutoka O-Lake mpaka kituo cha gesi ni zaidi ya mita 400, lakini ile foleni nyoka imezidi mita 500 na iko mistari mitatu na yapo magari yameshindwa kuingia kwenye foleni baada ya foleni hiyo kuingia barabarani, mstari ukinyooka kwa line moja unaitafuta km 2.
Katika stori na dereva huyu anayepaki na kushinda Airport, anasema wapo madereva wanavizia saa 7 usiku kwenda kupanga foleni ila wanafanikiwa kujaza saa 11 alfajiri, aloo masaa manne hayo tena huo ni usiku.. naona ukiipanga rush hours uombe ruhusa kwa HR kwamba kazini hutafika na kama mfanyabiashara usiifungue😉
Anyways mwaka jana Tanzania iliagiza mafuta lita bilioni nne na ni bidhaa inayofilisi fedha za kigeni, kweli Serikali imefikia mwisho wa kufikiri kurahisisha upatikanaji wa gesi? Maeneo ya Jeshi wanakojenga vituo vya mafuta kwanini wasijenge vituo vya gesi kuwarahishia wananchi wake!
Soma, Pia:
==> Msoto wa madereva kituo cha kujazia gesi Tazara jijini Dar es Salaam