Video: Hali ilivyo ziwa Victoria, magugu maji yalifunika ziwa na kuathiri usafiri Kigongo Busisi

Video: Hali ilivyo ziwa Victoria, magugu maji yalifunika ziwa na kuathiri usafiri Kigongo Busisi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kivuko MV. MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo Wilayani Misungwi na Busisi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kikikatiza katikati ya magugu maji wakati kikiwasili kwa ajili ya kupaki na kushusha abiria upande wa maegesho ya Kigongo.

Uwepo wa magugu hayo katika Ziwa Victoria eneo la upande wa Kigongo umekuwa ukisababisha adha kubwa kwa uendeshaji wa vivuko vya TEMESA vinavyotoa huduma katika eneo hilo.

Magugu hayo kwa nyakati tofauti yamekuwa yakivutwa na kuingia katika mashine za mbadilishano joto. (heat exchanger)

Magugu maji hayo yanaenda kuziba sehemu hiyo na kupelekea joto la injini kutobadilika na kupanda mpaka injini pamoja na jenereta za kivuko kuzima.

Kivuko MV. MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo Wilayani Misungwi na Busisi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kikikatiza katikati ya magugu maji wakati kikiwasili kwa ajili ya kupaki na kushusha abiria upande wa maegesho ya Kigongo.
Hapo ni pale lilipo daraja jipya?
 
Huwezi Amini, tuna Wizara ya uvuvi , Mali asili , uchukuzi n.k

Ila wapo tu bana, wanaangalia ,sisi kwetu Kila kitu ni mzaha
 
Kwani hua yanatumia muda gani kuota!!? Kua tangu linaanza jani, moja, moja wanayaangalia tu mpaka yanafikia hivyo
 
Tunasubiri Nchi wahisani/wafadhili waje watuletee mitambo/vifaa na kutufundisha kuyatoa.
 
NEMC,na uvuvi kazi Yao ni kufungia viwanda lakini kwenye haya ya magugu haliwahusu kabisa
 
Back
Top Bottom