SI KWELI Video hii imetengenezwa na Wasafi Media

SI KWELI Video hii imetengenezwa na Wasafi Media

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari wakuu, nimeshangaa sana kuona WASAFI TV ikitumia lugha ya kihuni tena yenye maudhi katika uwasilishaji wa taarifa.

wasafi-pic.jpg

Chombo mahili hakiwezi kutumia neno 'usela mavi' katika kufikisha ujumbe wake kwa hadhira,binafsi siyo mtaalamu wa teknolojia labda nyie wajuvi wa mambo hayo tazameni hii video chini kisha mniambie kama ni editing au laa.

Kama ni Wasafi kweli lazima tujiulize maswali yafuatayo:

Je hii jeuri wanaipata wapi ya kutudhihaki sisi juu ya msiba mkubwa kama huo?

Je wao wanatumika katika kuchochea maovu ya utekaji au wao wanajikuta akina nani labda na chombo chao?

Je wamezingatia nini katika uwasilishaji wao wa hiyo habari na je wameelewa kweli nini maana ya kupinga na kupaza sauti kwa vitendo juu ya mauaji?

Pia soma: Tafrani yazuka msibani Tanga: Waombolezaji wakataa dua ya Waziri Masauni wakimtaka ajiuzulu

Tunachokijua
Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA, Ali Mohammed Kibao Ijumaa ya Septemba 6, 2024 alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi ndani ya basi la Tashriff katika eneo la Tegeta mbele ya Jengo la Kibo Complex na siku moja baadaye mwili wake uliripotiwa kupatikana Ununio, jijini Dar es Salaam akiwa ameuawa huku akiwa ameharibiwa vibaya usoni mwake hali iliyopelekea kutokutambulika.

Mazishi ya Mzee Ali kibao yalifanyika mkoani Tanga na kuhudhuriwa na waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho ambapo baada ya mazishi hayo kumekuwa na Machapisho ya Video yaliyowekewa graphics yanayofanana kuwa ya Wasafi Media Yakielezea matukio mbalimbali kwenye msiba huo kupitia maandishi (Caption)

Ukweli upoje?
Utafutaji wa kimtandao kupitia Google Reverse Image uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hizo si za kweli na hazijachapishwa katika kurasa za mitandao rasmi ya kijamii za Wasafi TV wala Wasafi FM hivyo kuonesha poster hizo kuwa ni za upotoshaji kupitia Maandishi (Caption) yaliyoambatanishwa kwenye video ambazo ni halisi zikionyesha matukio mbalimbali kwenye Msiba wa Mzee Ali Kibao.

Aidha mpangilio wa nembo za mitandao ya kijamii katika poster hizo unatofautiana na mpangilio unaotumiwa na Wasafi TV pamoja na Wasafi FM, ambapo katika poster hizo mpangilio unaonesha facebook, Instagram, X, na TikTok tofauti na Mpangilio Halisi wa Wasafi unaoonesha nembo hizo kama Facebook, Instagram, X, Threads, Youtube na TikTok.

Vile vile post hizo hazina sehemu ya chini inayobeba nembo za mitandao ya kijamii yenye rangi ya bluu kama ilivyo katika poster za Wasafi TV na Wasafi FM. pamoja na tofauti hizo lakini pia neno Wasafi TV linalowekewa rangi nyekundu kwa nyuma katika Poster za Wasafi Media ni tofauti na poster hizo mbili ambazo zimewekewa rangi Nyeupe.

Video hizo zimechapishwa mtandaoni unaweza kuzipata hapa, na hapa.
Habari wakuu,nimeshangaa sana kuona WASAFI TV ikitumia lugha ya kihuni tena yenye maudhi katika uwasilishaji wa taarifa.

Chombo mahili hakiwezi kutumia neno 'usela mavi' katika kufikisha ujumbe wake kwa hadhira,binafsi siyo mtaalamu wa teknolojia labda nyie wajuvi wa mambo hayo tazameni hii video chini kisha mniambie kama ni editing au laa.

Kama ni Wasafi kweli lazima tujiulize maswali yafuatayo:

Je hii jeuri wanaipata wapi ya kutudhihaki sisi juu ya msiba mkubwa kama huo?

Je wao wanatumika katika kuchochea maovu ya utekaji au wao wanajikuta akina nani labda na chombo chao?

Je wamezingatia nini katika uwasilishaji wao wa hiyo habari na je wameelewa kweli nini maana ya kupinga na kupaza sauti kwa vitendo juu ya mauaji?
View attachment 3092166
Focus on what matters, yasikuhusu achana nayoo
 
Back
Top Bottom