The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Your browser is not able to display this video.
HAPA JAMAA ANAJITETEA BAADA YA KUTENDA NA KUISIKIA JAMII IKIMURUSHIA MADONGO...
Rais John Pombe Magufuli pamoja na kuwa ni aggressive, lakini sijawahi kumwona akishika kiboko kucharaza viboko watu hadharani...!!
Rais John Pombe Magufuli pamoja na kwamba hapendi wahalifu na matumizi mabaya ya rasrimali za nchi ikiwemo fedha, lakini hajawahi kuamuru wahujumu uchumi, watakatishaji fedha ama wezi wa mali ya umma wapigwe risasi ama viboko hadharani..!!
Rais John Pombe Magufuli, huponda na kufokafoka kwa maneno makali na ya kuudhi (sometimes) lakini huamuru uchunguzi kufanyika na hatua za kawaida za kikazi na kisheria kutendeka kwa wanaodhaniwa wamekosa...!!
Huyu DC yeye ni nani hasa hata afanye ujinga kama huu? Kwa kweli simuelewi na sijui kama nitamwelewa...!
Your browser is not able to display this video.
HAPA JAMAA ANATENDA UJINGA, ANATOA HUKUMU...
Laiti kama polisi wangejichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu wahalifu au washukiwa wa uhalifu sawa na mtazamo na akili za huyu DC, basi mpaka sasa ina maana kusingekuwa na haja ya kujenga magereza na kusingekuwa na wafungwa magerezani maana hukumu ingekuwa inatolewa papo hapo kwenye tukio...!!
Jamii hususani watoto tunaowaandaa kuwa viongozi wa taifa hili baadae wajifunze nini toka kwa kiongozi kama huyu DC anayejitetea kwa ujinga wa tendo lake?....
Je, jamii ijifunze na kuona kuwa kumbe ni sawa watu kujichukulia sheria mkononi kwa wanaowadhania ni "wahalifu" ama "wakosaji" kama alivyofanya DC?..
Kama mtazamo wa DC ndivyo ulivyo, kumbe basi, hakuna haja ya kuwa na mahakama Tanzania...
Baada ya kuona uhalifu huo, kila mtu angetarajia kumuona DC akiamuru watu hao anaodhani ni wahalifu ama wezi wakipelekwa mahakamani na kuadhibiwa kwa taratibu za kisheria..
Lakini hapa, looh, DC anadhani yuko juu ya sheria kwa kujiamulia yeye mwenyewe kutuhumu, kushika na kusikiliza kesi na kisha kutoa hukumu (adhabu) ya kuwapa....!
Sijui ni kwanini tu huyu DC mpaka sasa bado yuko ofisini maana amekosa sifa za kuwa kiongozi ktk nafasi hiyo asilani...!!