Video hizi 2 zinaongea lugha tofauti

Video hizi 2 zinaongea lugha tofauti

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
1. Video ya kwanza Rais Samia akihimiza wafanyabiashara watoe kodi kwa moyo kwani kodi haziingii mifukoni mwa Viongozi. Hapa anamaanisha serikali iko vizuri katika kubana matumizi.



Rais katika nia yako njema ya kulijenga taifa angalia na haya mambo madogo madogo, yanakula sana pesa za umma.

2. Video ya pili tunaona msururu wa magari zaidi ya 150 kwenye msafara wa Rais. Gari yoyote ili iingie kwenye msafara wa Rais lazima ikaguliwe (pesa inatumika), pili lazima ifanyiwe matengenezo ya kinga (service) hapa pia pesa inatumika.

Gari moja ndani ina dereva na watumishi wengine kadhaa wa umma, kila mmoja lazima alipwe posho, hapa pia pesa inatumika.

 
Kwenye hii nchi ukipata mwanya wa kukwepa kodi, hata usjiulize mara mbili. Maana kodi ya wananchi inayotumika kwenye matumizi sahihi ni sehemu ndogo sana.
Kiasi kikubwa huishia kwenye matumizi ya aina hii.
 
Back
Top Bottom