Video: Inasemekana Wimbo wa Rubby uitwao Na Yule ndo umekubalika sana Italy

ObieTrice

Senior Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
159
Reaction score
154
Msanii Ruby ameonyesha kufurahi sana baada ya mzungu kutoka italy akiimba wimbo wa ruby akapela uitwao na Yule. Rubby amepost akionyesha kufurahia sana. Wazungu wa Italy waliupokea vizuri sana wimbo huo hata na wengine kuimbaimba na kupost videos kuonyesha upendo kwa msanii huyo. Hii ni moja ya video ya mzungu kutoka Italy akiuimba japo hajui kiswahili..

 
nandy yuko vizuri
nyimbo zake zina utunzi mzuri zaidi ya ruby...
ruby pia yuko vizuri
wasanii wetu wa kike wako vizuri wote nawapenda
 
Duh kweli Italy wamemkubali [emoji16][emoji16]
 
Kweli ruby ni zaidi ya Nandy.


Sio Nandy tu, Jay Dee, Vanessa Mdee na mademu wengine wa Bongo Flava wanasubiri kwa Ruby.
Ruby kwa kuimba alazimishi, ni natural kama ilivyo kwa Saida Karoli.
 
Ndio hayo tunayoyasema. Nandy hawezi kumkaribia hata kidogo Ruby. Tatizo kuna wachache wameshikilia mziki wanafanya juu chini kumshusha mtoto wa watu huku kwenye public wakihubiri kataa kuwa kaa. Huu ni uhuni.
Siamini...
Kuna redio efm, uhuru, east africa redio, passion, radio free africa, redio za mikoa unataka kuniambia ana zicontrol ruge?
Naona tatizo kubwa ni kwamba anajua kuimba anasauti nzuri ila watunzi.
Maana nyimbo zake zote za awali aliandikiwa na watu hasa wa THT, sasa kakorofishaba na uongozi ndiyo hivyo kila nyimbo anayotoa watu sijui hawazielewi...
we mwenyewe si ajabu zaidi ya nyimbo alizotoa alipokuwa hajakorofishaba na clouds hakuna wimbo wake mpya unaoujua wakati ashatoa nyimbo kama tatu ikiwemo singeri
 
Sasa wewe ndio unanilaumu mimi!!? Mimi nasema ninachoona na wewe sema ujuacho. Nasikia Ruby na Ruge wanasali kanisa moja na eti Ruge alimtoa kanisani na kumpeleka THT baada ya hapo ndio akampotezea kutokana na ucha Mungu wake wa kutenda mema na kutokuwa Yezebeli.
Sasa hapo kaa ni nani?
 
Ruby alipatikana kwenye mashindano ya kuimba ya fiesta super nyota na alikuwa mshindi wa dar baadae akawa kati ya washindi wa kitaifa, yani kama ilivyo kwa akina young killer, stamina na wengine.
Ila ni kweli alikuwa akiimba gospel kanisani
 
Ruby alipatikana kwenye mashindano ya kuimba ya fiesta super nyota na alikuwa mshindi wa dar baadae akawa kati ya washindi wa kitaifa, yani kama ilivyo kwa akina young killer, stamina na wengine.
Ila ni kweli alikuwa akiimba gospel kanisani
Je, haiwezekani kuwa kupitia mashindano ni ujanja ujanja tu. Kwanini Ruby washindwane na Clouds?
Ruby anamadhara gani? Kwanini wazifungie nyimbo zake? Kama siyo kuwa kama kaa?
Wenyewe wanasema kataa kuwa kaa wakati wao ndio makaa. Kwanini ukipoteze kipaji hicho.
Unaweza kuniambia kwanini nyimbo za Ruby hazipigwi Clouds wakati ndio wao walimuibua?
 
Hivi wewe ukiwa unamiliki redio bila unafiki sema ukweli mimi ni msanii tumeshindwa kuelewana labda unadai nakulipa pesa ndogo, then nisiishie hapo niende nikuandike mbovu utaendelea kupiga nyimbo zangu?
Mimi swali ninalo jiuliza kuacha clouds kupiga nyimbo zake kuka comnection gani na yeye kushuka wakati clouds ni redio moja tanzania kuna utitiri wa redio kibao?
Kuna kipindi alikuwa akifanya media tour redio na tv mbalimbali alikuwa katoa nyimbo mpya kwanini nao hawazipigi?
 
Hilo swala lako mbona umeshalijibu wewe mwenyewe.
Halafu hebu niambie tatizo la msingi kati ya Ruby na Clouds.
Bila kuwa biased nani mwenye makosa kati ya Clouds na Ruby?
 
Hilo swala lako mbona umeshalijibu wewe mwenyewe.
Halafu hebu niambie tatizo la msingi kati ya Ruby na Clouds.
Bila kuwa biased nani mwenye makosa kati ya Clouds na Ruby?
Siwezi kujua nani mwenye makosa maana kati yao hakuna ambaye aliwahi kusema hadharani tatizo ni nini zaidi ya kuona ruby anatupia vijembe mtandaoni na ruge akajibu yeye hana tatizo na ruby na kipindi ruby alikuwa kaitwa coke studio kwasababu ya clouds na aliyemsindikiza ni mfanyakazi wa clouds.
So kama unakubariana na mimi kuwa ana tatizo la utungaji basi clouds wasilaumiwe kuwa wanamshusha, aambiwe yeye kuwa atafute mtungaji wa nyimbo na melody nzuri tofauti na THT ambao kwa sasa hawawezi kumtungia nyimbo.
Hata wewe msipoelewana na mtu kuna vitu huwezi kumfanyia tena
 
Nimekuuliza ni nani mwenye tatizo? Umeshindwa kusema ni nani mwenye tatizo. Halafu hapo hapo unamhukumu Ruby.
Kwani ukiwa muimbaji lazima uwe unaandika nyimbo. Kwanini Clouds watumie nguvu waliyonayo kumnyanyasa asiye na uwezo?
Nakuuliza tena Kati ya Ruby na Clouds nani mwenye matatizo? Kama hujui chochote huna haki ya kuhukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…