KWELI Video inayoonesha gari ndogo inapanda mlima mkali kwa spidi kubwa ni halisi

KWELI Video inayoonesha gari ndogo inapanda mlima mkali kwa spidi kubwa ni halisi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Wakuu salaaam

Hivi hii video ni ya kweli au wanatupiga hapa, hiyo gari inaweza kweli kupanda mlima mkali kama huu

Screenshot 2024-11-07 102132.png


 
Tunachokijua
Mashindano ya kuendesha magari kwenye miinuko yenye mchanga kwenye nchi za Uarabuni yanajulikana kama Dune Bashing au Desert Rally. Haya ni mashindano maarufu ambayo yanahusisha magari ya aina ya 4x4 kuendeshwa kwenye mchanga wa jangwa, hasa katika miinuko ya matuta ya mchanga (dunes).

Mashindano haya hufanyika katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati kama vile Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, na Oman. Dune Bashing ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii wa jangwani, na pia kuna mashindano rasmi kama vile Abu Dhabi Desert Challenge na Dubai International Baja, ambayo yanahusisha mbio ngumu kwenye mazingira ya jangwa.

Aina nyingine ya mashindano ni Rally Dakar, mashindano makubwa ya kimataifa ambayo mara nyingi hushirikisha vipengele vya kuendesha kwenye jangwa na mchanga.

Kumekuwapo na Video ikionesha gari aina ya ..... ikipanda mlima wenye mchanga kutoka chini mpaka juu kileleni.

Je, Video hiyo ni halisi?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo ni Halisi na haijatengenezwa kwa akili mnemba(AI). Video hiyo iliwekwa mtandaoni kwa mara ya kwanza January 29, 2023 , kwenye mtandao wa Instagram na akaunti ijulikanayo kama hlx_2700 ikiwa na maelezo kwa lugha ya Kiarabu ambapo kuna magari ya aina mbalimbali kama vile Hilux, Patrol, Chevrolet, na Lexus na mengineyo kwenye hayo mashindano ya jangwani au "Dune Bashing".

Aidha, Video hiyo inaonesha gari aina ya Pick up likitimua vumbi ambalo kwa teknolojia ya akili mnemba haliwezi kutengenezwa bado, mwanga uliosawia na magari yaliyo katika hali ya kawaida hali inayothibitisha uhalisia wa video hiyo kuwa ya kawaida na si ya kutengenezwa.

screenshot-2024-11-07-102132-png.3145943

Ni kwel n Gari ndogo lkn c ist mkuu
 
Hiyo ni Toyota Land cruiser Pick up 4.0L V6 Engine,
Bei yake sio chini ya Tsh 104+ M

Inapanda bila tatizo kabisa.
 
Back
Top Bottom