Ukiangalia kwa makini hii ni 'propaganda'' ya kafulila. Nimesikiliza sehemu yote sikumsikia mgombea wa Chadema isipokuwa katika maswali na majibu. Anyway, kuna hata ninayoona yana uwalakini.
1. Katiaka agenda nne za Kafulila suala la afya hakulitaja na kwahiyo halipo katika agenda za chama chake. Ametaja afya katika majibu baada ya kumsikia Hassanali akisema agenda zake ni Afya,Elimu na kilimo. Hili linatosha kuonyesha kuwa Kafulila ni ''ambitious but not objective''
2.Kafulila kasema ataanzisha mfuko wa jimbo wa elimu na atachangia 30% ya mshahara wake. Tatizo la maendeleo haliwezi kutatuliwa na fedha za mtu mmoja. Hii ni ghilba kwa wananchi kwasababu 30% ya mshahara wa Mbunge kimaandishi ni apprx 600,000 sawa na posho za siku 4 za mbunge Dodoma. Huu ni udanganyifu kwasababu posho za wabunge zinafikia Mil 8.[kukwepa kodi, eti mshahara ni 2M]
3. Amesema atatumia ushirika kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima wapate mikopo ya umwagiliaji. Kafulila nenda Kilimanjaro ukaone, watu wamekuwa na irrigation schemes Milimani kabla ya mjerumani hajaja. Tatizo la irrigation sio pesa ni mwamko na uelewa wa watu. Kama watu hawajui kwanini wanatakiwa kuwa na irrigation scheme, pesa haziwezi kusaidia lolote. Kafulila anadhani maendeleo ni pesa!
4. Ametaja serikali shirikishi kama agenda, hakufanunua shirikishi kivipi na itasadia vipi kumkomboa yule mwananchi maskini asiye na elimu na mwenye afya mbaya pale kigoma.
5. Amesema kigoma ilitoa manamba wengi kwasababu walikuwa na nguvu. Huu ni uongo wa kiwango cha juu. Kama wangekuwa na nguvu kuliko watanzania wengine basi tungewaona enzi hizo wakiwa katika ajira kama polisi au majeshi. Kafulila, watu wa kigoma walikuwa manamba kwasababu ya uduni wa elimu. Elimu iliwafanya wawe wanyonge hata mbele ya watanzania wenzao. Nenda katika mikoa yenye mabaki ya kambi za manamba, utagundua kuwa hali za maisha kwenya kambi za manamba ni duni licha ya nguvu za watu wa sehemu hizo. Ni sehemu ambazo elimu ni duni sana, kafulila nenda Tanga utathibitisha ninayosema. Manamba anaowasifu kafulila walikuwa exploited na watanzania wenzao kwasababu ya kukosa elimu. Kama kukosa elimu ndio nguvu anyozungumzia kafulila, basi hoja yake ni kweli vinginevyo arejee maktaba kutafuta ukweli.
Kwa mtazamo wangu ambao si lazima umpendeze kila mtu, kafulila hafai kuwa mbunge, hana vision, ni kasuku aliyekariri mistari. Siwezi kumfananisha kafulila na J.Mtatiro, J.Mnyika, Z.kabwe, H.mdee. kwa uchache. Katika nchi kama Tz huwezi kuwa na agenda bila kutaja afya! Kafulila kabeba ilani ya chama chake bila kujua matatizo ya watu wake. Ninachoweza kumsifu kafulila ni uwezo wa kuongea kama mwanasiasa kwa mikono na misemo. Ningependa sana kuwa na wabunge wapinzani wengi,lakini si akina Kasuku Kafulila! Ni mtazamo wangu.