Leo Oktoba 17, 2025, hafla ya kuuaga mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, inaendelea katika Uwanja wa Nyayo, ikihudhuriwa na Rais William Ruto, viongozi mbalimbali, familia pamoja na wananchi
Katika hafla hiyo Kaka wa Raila Odinga, Seneta Oburu Odinga ambaye kwa sasa ndiye Kiongozi wa Chama cha ODM, alipopewa nafasi ya Kuzungumza aliwatambulisha wake zake wawili
“Kwa umri wangu huu, sitaki mke wangu wa kwanza ahangaike ndiyo maana nikamleta msaidizi wake, Judith Oburu…” amesema Seneta Oburu Odinga akimtambulisha mke wake wa pili