Video: Kesi ya F. A. Mbowe na wenzake, wakili aichambua hukumu ndogo ya Jaji M. Siyani...

Ulivyoandika utadhani mbowe ni malaika.
 
Dhuluma na maovu yafanywayo na hii Serikali hayana tofauti kabisa na dhuluma na maovu yaliyofanywa na iliyokuwa Serikali ya Makaburu wa Afrika Kusini.
Seriously, mimi naomba mwenye fikra tofauti juu ya haya uliyoweka hapa aje aeleze tofauti iliyopo kati ya utawala wa Makaburu na hawa CCM wa Tanzania.
Tofauti itakuwa ni kwenye rangi za ngozi za wahusika tu basi.
 
Mama anaona kabisa katika hii NCHI hakuna shida. Ipo siku
Mkuu 'Akasankara', siyo kwamba "Mama anaona kabisa katika hii NCHI hakuna shida" peke yake, kuna jambo la msingi zaidi ya kuona shida tu!

Kidogo inashangaza, kuna shida kubwa na watu waliopo huko kwenye utawala, wanaotoa ushauri na wanaotekeleza ushauri wenyewe!

Kila mtu anajuwa kesi ipo mahakamani, inaendelea, utawala unaamua anayesikiliza kesi hiyo azawadiwe, hata kabla ya kesi haijaamuliwa.

Hivi, katika hali ya kawaida, huwezi mtu/kiongozi ukasita kidogo kufanya baadhi ya maamuzi, angalao kwa muda ili usiweke mazingira ya kuonekana unaingilia maamuzi ya kesi?
Hata kama unajuwa uwezo wa kufanya hivyo unao, kule tu kujionyesha kwenye kadamnasi kufanya jambo kama hilo, halistuwi/tahadharishi hawa viongozi?
Hawa ni watu wasiokuwa na staha katika matendo yao? Hawajali wanaowaongoza watayachukulia vipi maamuzi yao?

Hawa sasa wamekuwa ni "sikio lisilosikia dawa." Wao sasa wanajiona wanaweza kufanya lolote wapendalo kufanya bila kujali kama matendo yao yatakuwa yanawafunua kuwa ni viongozi wasiostahili kuliongoza taifa hili.
 
Huyo Judge huko aliko, likaptula limelowana, labda leo atalala na pampers maana ni zamu yake kunywa maji....
 
Ni kwa sababu NAFSI YAKE IMEBEBA HATIA [guilty conscious]. Anaona giza mbele yake. Anamtumikia ibilisi shetani. Na shetani hana mzaha, atamtumikia weeeee lakini mwishoni anammaliza kwa kumchinja yeye. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu Kristo...!!

Hapo awali alijitahidi sana kuonekana ni mtu wa haki lakini mwizi ni mwizi tu japo atajifanya kuvaa ngozi ya mwanakondoo asiye na dhambi lakini mwisho wa siku atajionesha tu kwa ngozi yake halisi ya chui....
 
si mahala pake- wanashindwa kutoa ushahidi mahakamani wanaleta kelele huku- bure kabisa

jaji: Kuhusu Pingamizi la pili kuhusiana Adamoo kulalamika kwamba Ameteswa

jaji: Wakili wa Serikali amesema Maelezo hayo yaliandikwa Siku ya tarehe 07 Mwezi wa 08? Na Kwamba Upande wa Utetezi wameshindwa Kuibua shaka.

jaji: Upande wa Utetezi umeshindwa Kuwahoji Mashahidi wa Jamhuri

jaji: Maelezo ya Adam Kasekwa ni kwamba Japo alitoa Maelezo lakini hakutoa kwa ridhaa yake.

jaji: Kuhusiana na Ushahidi wake hauonyeshi kuwa alitoa Maelezo au Kuteswa akiwa Central Police Dar es Salaam.
 
Maelezo haya ya Jaji na wewe kuyakwoti na kuyaleta hapa ukiyalinganisha na ya wakili huyu na tuliokuwepo mahakamani siku zote kufuatilia mwenendo wa kesi ni tofauti na mbali kabisa kama ilivyo mbingu na nchi....!!

Jaji ametoa hukumu yake kwa kudhani na kwa hisia zake akiacha ushahidi wote wa mashahidi wa upande wa utetezi ukielea hewani...

Yaani, Jaji Mustapha Siyani kama alivyofanya mtangulizi wake Jaji Luvanda, naye kaamua kuegemea na kusaidiana na upande wa mashitaka. Kwa ufupi ni kuwa, Jaji Siyani kaacha jukumu lake la kuwa MWAMUZI ANAYEONGOZWA NA SHERIA ZA MCHEZO ili kuamua kwa haki, kaamua kuwa mchezaji wa moja ya timu na wakati huo huo akipuliza na kipyenga...!!

Yana mwisho haya...
 
Hivi mbona sheria ikiwawajibisha wapinzani inaonekana wanaonewa ila ikiwawajibisha kina Sabaya inaonekana inatenda haki
 
Amejitoa kuisikiliza kesi hii kwa maumivu makali katika nafsi yake kwa kuisigina haki mchana kweupe akidhani kwa kuwa yeye ni JAJI, wengine wote ni "wajinga" hatutaona upuuzi wake. Amekosea sana...!

Huyu kajitoa si kwa sababu eti ya majukumu yake mapya ya ujaji kiongozi, la hasha...!

Ni kwa sababu NAFSI YAKE IMEBEBA HATIA [guilty conscious]. Anaona giza mbele yake. Anamtumikia ibilisi shetani. Na shetani hana mzaha, atamtumikia weeeee lakini mwishoni anammaliza kwa kumchinja yeye. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu Kristo...!![emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
jaji: Upande wa Utetezi umeshindwa Kuwahoji Mashahidi wa Jamhuri

Jaji kabainisha wazi kuwa mawakili wanaharakati walishindwa kuwahoji mashahidi wa Jamhuri ili kuthibitisha madai yao.
Hili liko wazi kwenye mwenendo wa wa kesi- kumbuka kwa mfano
wakili- wewe unaitwa Mahita
shahidi- Ndiyo
wakili- Mtoto wa Omary Mahita IGP msataafu
Shahidi- Ndiyo
Wakili- Baba yako aliwahi kuwasingizia CUF tuhuma za ugaidi

OFF POINT KABISA
 
Naona unahangaika kuokoteza vipande vinavyokufurahisha visivyo na maana kisheria, vile vya PGO mbona huviweki?
 
Hadi sasa nasubiri ushahidi usio na shaka ambao kamanda mkuu Sirro alibainisha upo...

Hii kesi ndogo hukumu yake tayari ni chenga...
 
Tatizo lako unachungulia dirishani badala ya kuingia ndani uione nyumba ktk engo zake zote...

Sijui kama unaweza kunielewa. Kama hujaelewa, waulize walio jirani zako wakueleweshe...
 
Kisheria inaruhusiwa kukata rufaa ?
Hapana, siyo ktk hatua hii...

Hii ilikuwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within trial)...

Rufaa inaweza kukatwa iwapo kesi ya msingi itaamuliwa na hukumu yake iwe na mwelekeo kama huu wa kesi hii ndogo...

Lakini hata kama hukumu itamwachia Freeman Mbowe na wenzake huru, maamuzi ya kesi hii ndogo LAZIMA yakatiwe rufaa ili kurekebisha precedence mbaya ya kuja kuumiza watu wengine huko mbeleni...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…