Mkuu 'Akasankara', siyo kwamba "Mama anaona kabisa katika hii NCHI hakuna shida" peke yake, kuna jambo la msingi zaidi ya kuona shida tu!
Kidogo inashangaza, kuna shida kubwa na watu waliopo huko kwenye utawala, wanaotoa ushauri na wanaotekeleza ushauri wenyewe!
Kila mtu anajuwa kesi ipo mahakamani, inaendelea, utawala unaamua anayesikiliza kesi hiyo azawadiwe, hata kabla ya kesi haijaamuliwa.
Hivi, katika hali ya kawaida, huwezi mtu/kiongozi ukasita kidogo kufanya baadhi ya maamuzi, angalao kwa muda ili usiweke mazingira ya kuonekana unaingilia maamuzi ya kesi?
Hata kama unajuwa uwezo wa kufanya hivyo unao, kule tu kujionyesha kwenye kadamnasi kufanya jambo kama hilo, halistuwi/tahadharishi hawa viongozi?
Hawa ni watu wasiokuwa na staha katika matendo yao? Hawajali wanaowaongoza watayachukulia vipi maamuzi yao?
Hawa sasa wamekuwa ni "sikio lisilosikia dawa." Wao sasa wanajiona wanaweza kufanya lolote wapendalo kufanya bila kujali kama matendo yao yatakuwa yanawafunua kuwa ni viongozi wasiostahili kuliongoza taifa hili.