Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mama Gift, mkazi wa Kitongoji cha Mbugani, Kijiji cha Magugu wilayani Babati, amenusurika kushambuliwa baada ya kudaiwa kukutwa usiku akifukia dawa zinazohusishwa na imani za kishirikina katika nyumba ya jirani.
Mwanamke huyo mara baada ya kugundulika na kijana anaye fahamika kwa jina la Idrisa Mohamed amesema alimkuta Mama huyo akiwa tayari ameshafukia dawa kisha akaondoka na kurudi tena huku akipewa maelekezo ya sehemu alipo fukia dawa hiyo hapakuwa sahihi mara baada ya kugundulika mwanamke huyo alianza kumshambulia kijana huyo kwa kutaka kumchoma na kisu,
Baadhi ya wananchi waliofika katika eneo hilo wameshtushwa na tukio hilo kwani mwanamke huyo amejikita sana katika Maombi pamoja na uimbaji wa kwaya tukio lililowaacha wanananchi wengi midomo wazi wamesema mwanamke huyo amekuwa msumbufu kwa matukio kadhaa huku wakikemea vikali tabia hizo,
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha mbugani Jonasi Daudi amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema alipokea taarifa hizo majira ya saatisa kasoro za usiku ndipo alipofika katika eneo la tukio na kumkuta mwanamke huyo akiwa utupu na mara baada ya kuhojiwa mwanamke huyo alikiri kwa kusema alikuja kuroga na kuhisi kuwa alitupiwa magonjwa na jirani yake ndipo alipo chukua jukumu la kwenda kuchimbia dawa hizo.
https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/share/v/1EJfSL1Ztg/
Naona umekuja kumtetea mwenzio.Hakuna mlokole ambaye anawanga. Ulokole ni kinyume na kuwanga. Automatically mtu anapoanza kuwanga anakuwa ameacha ulokole ikiwa alikuwa mlokole. Ni sawa na kusema Padre na mke wake . Tunajua Padre huwa haoi. So anapooa tu anakosa sifa ya Upadre
Ndio hao wanaochanganya mambo, walokole wa kweli hawachanganyi mamboTukisema Walokole wana matatizo makubwa mnabisha
Wote ni wagonjwa tu, hata mirembe kuna madarajaNdio hao wanaochanganya mambo, walokole wa kweli hawachanganyi mambo
Pressure ya utajiri, kila mtu anataka kuendesha G-wagon ππhaya mambo ya kishirikina siku hizi kuna watu wanadiriki mpaka kuvuk mito na bahari kwenda kununua uchawi.
yani siku hizi katika watu 10, basi wanne ni wachawi au wanajihusisha sana na maswala ya kishirikina.
Bado nafanya uchunguzi kutaka kufahamu kwa nini siku hizi uchawi na ushirikina vimetamalaki sana hasa kwa vijana below 45 years of age.
mbona pamoja na juhudi zote za uchawi lakini bado hatuzioni mtaani? ujinga tu. wanitafute niwapeleke kwa mwamba wangu flani yupo malawi huko. hana mbambamba. unakua na pesa mpka unaanza kuzikimbiaPressure ya utajiri, kila mtu anataka kuendesha G-wagon ππ
Hydroxoio inakutoka tu hapo ulipo maana hujui hata falsafa au dhana ambayo nimeijenga kwa hoja...Naona umekuja kumtetea mwenzio.
Nguvu inatumika sana , utalia mwaka huu . π π Wanga wote ,wachawi wavaa suti yaani yote manabii , mwamposa , kakobe , suguye , malisha kama wote ..Museven kawaita juzi kuombe wagonjwa wa Ebola , wamekimbia kama sio wao .Hakuna mlokole ambaye anawanga. Ulokole ni kinyume na kuwanga. Automatically mtu anapoanza kuwanga anakuwa ameacha ulokole ikiwa alikuwa mlokole. Ni sawa na kusema Padre na mke wake . Tunajua Padre huwa haoi. So anapooa tu anakosa sifa ya Upadre
Huo ni mtazamo wakoWote ni wagonjwa tu, hata mirembe kuna madaraja
Ndivyo walivyo, na ndivyo ilivyo.Huo ni mtazamo wako