Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mtanzania mwenye umri wa miaka 33, Fatma Nassoro anapitia mateso makubwa akiwa nchini Iraq, ambako alienda kufanya kazi tangu mwaka 2022. Fatma amesema amekuwa akiishi katika mazingira magumu chini ya mwajiri wake, huku akinyimwa chakula, kupigwa mara kwa mara, kutukanwa, kubezwa, na hata kutemewa mate.
Juhudi zake za kutaka kurejea nyumbani zimegonga mwamba baada ya mwajiri wake kuficha pasipoti yake, akimzuia kuondoka. Mwaka jana, Fatma alipata msiba mzito baada ya kufiwa na mtoto wake, lakini alinyimwa ruhusa ya kurudi Tanzania kuhudhuria mazishi.
Kwa sasa, hali imezidi kuwa ngumu, huku afya ya mama yake ikiwa dhoofu, lakini bado ameshindwa kurudi kumwona. Fatma anasema Iraq haina ubalozi wa Tanzania, hali iliyomwacha bila msaada wa karibu wa kisheria au ulinzi.
Amebainisha kuwa anawasiliana kwa siri kupitia namba ya jirani wakati mwajiri wake hayupo, akitafuta msaada wa kurejea nyumbani. Fatma anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania na mashirika ya haki za binadamu kumsaidia kurejea salama na kumaliza mateso anayopitia.