Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Athletic Bilbao walipochuana na timu ya vijana yenye wachezaji 100 Tuesday, May 25, 2010 2:44 AM
Ilikuwa ni mechi ambayo haijawahi kutokea duniani, wachezaji 11 wa timu ya Athletic Bilbao waliingiwa uwanjani kucheza na timu yenye wachezaji 100 na magolikipa watatu. Mwisho wa mechi Bilbao walishinda 5-3. Washabiki 20,000 walikuwepo uwanjani kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa maalumu kwaajili ya kuchangia pesa kwa mashirika ya hisani na kumuaga mchezaji wa Athletic Bilbao Joseba Etxeberria, 32, ambaye anaondoka kwenye timu hiyo baada ya miaka 15.
Timu ya Ahtletic Bilbao ikiingiza uwanjani kikosi cha mastaa wake wa ligi kuu ya Hispania walicheza kwa kutumia fomesheni yao maarufu ya 4-4-2 lakini timu pinzani yenye vijana 100 ilitumia fomesheni ya 20-60-17.
Ilikuwa ni vigumu kuuona mpira upo wapi kutokana na msongamano wa wachezaji uwanjani na haijulikani ni wachezaji wangapi walifanikiwa kuugusa mpira.
Pamoja na kwamba timu yenye wachezaji 100 ilikuwa na magokipa watatu kwenye lango lake, ilitoka uwanjani ikiwa imefungwa 5-3.
Chini ni VIDEO ya mechi hiyo.
VIDEO - Mechi Ambayo Haijawahi Kutokea Duniani
Kuiona hiyo Video bonyeza hapa NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
http://javascript<b></b>:__doPostBack('LinkButton3','')