Kwanini lakini?
Mnatusaidia ili tuwape shukurani? Au ndiyo ulimbukeni huo?
Hakuna msaada wa lazima, hizo pesa mnazotoa mnawapa wahafidhina kwa maslahi yenu wenyewe. Kama mna hamu ya kusaidia mbona mnawaondosha wakimbizi kwa nguvu? Hebu tuachieni basi
Ndugu yangu, Tanzania ni nchi pekee iliyowahi kutoa Uraia kwa wakimbizi 160,000 katika historia ya dunia kwa wakati mmoja tu.
Achilia hayo Tanzania imetoa msaada kwa nchi zote ikiwa ni pamoja na kuwahifadhi wakimbizi.
Hatufukuzi wakimibizi kwasababu tunao wakimbizi wa zanzibar wapatao 350,000, itakuwa ni uonevu kuwafukuza Wanyarwanda 80,000 tena wasiotumia rasilimali yoyote kama wale 350,000.
Kuhusu kuachiwa, nadhani wewe ni mgeni katika ukumbi huu. JF wametoakila aina ya msaada ili 'muachiwe''.
Wazanzibar wamebaki na muungano wa mkataba hawataki kusikia neno vunja muungano. Nani king'ang'anizi?
Umemsikia Mansour akikiri kwa ulimi wake kuwa wanataka muungano, sasa mtu anayetaka muungano aachiwe kivipi tena wakati yeye anautaka muungano!
Umemsikia Mansour anasema anataka mkataba, sasa mkataba wa nini nanyi mnataka kuachiwa. Utaachiwaje ukiwa katika mkataba.
Mansour amesema anataka ushirikiano katika ulinzi. Hii maana yake ni kuwa wanataka wapewe ulinzi wa bure kama wanavyopewa elimu, nishati na mishahara.
Mansour amejichanganya aliposema mkataba wa mzee Karume ndio wanaoutaka. Sasa mkataba wa muungano ni wa nini tena wakati wa mzee Karume upo bado?
Anasema ZNZ inataka self determination, endapo wanataka hivyo kwanini anaomba mkataba wa muungano tena.
Katika kuonyesha kuwa ZNZ ina viongozi wa ajabu na ambao hatujui uwaziri wanaupataje, Mansour anasema hataki kusikia faida za muungano wa mbatata na vitunguu. Hapo hapo analalamika kuwa watu wa jimboni kwake hawawezi kuingiza TV bara aua Magari. Mansour anafahamu kuwa katika makontena 800 yanayopakuliwa ZNZ 750 yanabeba bidhaa kwa soko kubwa la Tanganyika. Kiongozi huyu asiye na maono halioni hilo kama faida ya muungano.
Sijui amesoma wapi, ninachojua ni kuwa asilimia 98 ya WZNZ viongozi na wafanyakazi wamesoma kwa kodi za Mtanganyika tena bure na nafasi za upendeleo hata kama alikuwa kilaza. No wonder ndio maana tuna majuha kama Mansour
Mnasour amesema anataka muungano kama wa EU. Sijui ZNZ inasomesha nini huko skuli maana EU ni jumuiya na si muungano. Kwa mantiki hiyo anachokiataka ni kuwa na EAC au SADC. Lakini kwa kuhofia neno vunja muungano bado Wazanzibar wameng'ang'ana na muungano wa mkataba ambao sisi tunasema mwisho ni Chumbe.
Upuuzi huo hautavuka bahari, na ukivuka uvushwe na Wazanzibar kwa sharti kuwa Adabu na heshima mbele, kidomo domo mwisho chumbe.
Anasema EU kuna wanachama wenye nchi zenye watu 20,000. Huu kama ndio uzanzibar na usomi wa ZNZ basi kuna tatizo zaidi ya muungano. Hivi huyu juha anajua EU kweli.
Halafu anasema anataka muungano wa haki na usawa, sasa nani anayetakiwa adai haki, yule anayening'inia mgongoni au yule aliyembeba? Halafu Mansour na elimu yake hajiulizi bajeti yake ya miaka 10 ni sawa na kusanyao la mwezi la Tanganyika, usawa utatoka wapi?
Kama alivyo Ahmed na Maalim Seif, Mansour ameshindwa kutaja hayo mambo ya mkataba ni yapi. Ameishia kutueleza kuhusu Hong Kong na Makao, sijui kama huyu Waziri wa Kizanzibar aliwahi kukaa darasani na kusoma historia, jiografia na elimu ya uraia. Huwezi kufananisha chungwa na matembele waziri Mansour! Too low kwa waziri.
Mwisho, Wazanzibar wakae wakielewa kuwa muda wa kuwaendekeza na mdomo juu sasa basi.
Zanzibar inaihitaji Tanganyika kwa namna yoyote ile ndio maana wamepewa panga hakuna anayethubutu kulitumia.
Hakuna anayesimama na kusema vunja muungano, wamebaki kuitisha makongamano ya kudanganyana.
Tanganyika tunasema ZNZ hamna haki ya kuchagua aina ya muungano kwasababu muungano wowote ule ninyi kama ZNZ hamuwezi kuweka kitu cha maana mezani. Kwa bilioni 10 kwa mwezi mna kitu gani. Si afadhali tufanye muungano wa mkataba na Bakhresa!
Muungano mnaoutaka ni kuhemea na hapo ndipo tunajeuri ya kuwaambia bila kificho Tulieni mapakatwe! Mumeshindwa kutamka neno vunja muungano hamna lolote la maana la kusema zaidi ya hadithi. Hadithi mwisho chumbe! ukivuka bahari kama wale 350,000 adabu mbele, heshima kwanza.
LET ZNZ GO!