Video: Ronaldo ajigeuza ombaomba mtaani

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,455
Mtazame Ronaldo alivyojigeuza ombaomba huku akicheza mpira ndani ya Madrid, alijigeuza babu watu wakampotezea baada ya kumjua ikawa mafuriko wanataka kupiga nae picha,

https://youtu.be/RKr-U1r1AlM
 
Na kweli...nadhani hajafanya just for fun...!

Umeona eeeh yaani ombaomba mwenye kipaji kadharauliwa tu lakini maajabu ni kwamba watoto hawana kitu ubaguzi katika nafsi zao labda wajazwe chuki...
 
wengi walimdharau na kuona si chochote. baada ya kuvua ile sura bandia kila mtu anampigia makofi wanamzonga. Mtoto alistahili ile zawadi ya mpira, hakujali kucheza na "mjinga"
 
Tupe faida na sisi farkhina

Yaani nimeona vitu viwili reputation and talent

Watu wanampenda ronaldo kwa talent yake au reputation alionayo ijapokua inatokana na talent

What if angekua homeless kama alivyo act? Kipaji chake kisingeonekana
 
Last edited by a moderator:
Aiseee jamaa baada ya kutoa nywele zake ndo watu wanamfata.. alipokuwa hana hadi namba kanyimwa..... tena straight No sorry
 
Kweli kabisa farkhina binadamu wa ajabu sana, Muda wote kaonyesha talent yake hakuna alojali zaidi ya mtoto, lakini alipojivua hizo ndefu kwa sec tu hakuna njia ya kupita
 
Last edited by a moderator:
wengi walimdharau na kuona si chochote. baada ya kuvua ile sura bandia kila mtu anampigia makofi wanamzonga. Mtoto alistahili ile zawadi ya mpira, hakujali kucheza na "mjinga"

Kuna msemo unasema aso kitu si mtu,ni kutokana na watu wanavyowadharau wenye hali duni
 
Umeona eeeh yaani ombaomba mwenye kipaji kadharauliwa tu lakini maajabu ni kwamba watoto hawana kitu ubaguzi katika nafsi zao labda wajazwe chuki...
Jingine japo halipo wazi sana...tunafanya mambo mengi kwa ajili ya watu maarufu(kuwashabikia n.k)...lakini tunashindwa kugawa muda kidogo japo kujumuika na hao ombaomba...(hata kwa kuwaonesha upendo tu....)
Alipojiweka kama ombaomba hakuna aliyesogea lakini walipomgundua wakamshabikia sana...
 
Wote tunazaliwa bila chuki.. ila zinapandikizwa tu. Yule mtoto huenda ndio katoka kimaisha hivyo maana kukubali kucheza mpira na ombaomba maana anakipaji ila pakutokea ndio shida. Na hapo amepata pa kutokea amini hivyo
 
Concept nzuri sana hiyo, watu watakuthamini ukiwa na kitu but viceversa itaishia kuiona dunia sio sawa kwako but GOD IS GREAT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…