The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Mengine yaliyopita yote tunayaelewa...
Hapa nimerudia kumtazama na kumsikiliza mara mbili tatu, sijafanikiwa kumwelewa kabisa. Kwangu mimi namuona kama mtu aliye "so desperate and confused". Hajali sheria wala taratibu ama katiba ya nchi tena...
Spika Ndugai na wenzake huko CCM chini John Pombe wanataka wapate chochote kwa njia yoyote haramu ama halali. Wako tayari kutoheshimu sheria na katiba ya nchi waziwazi kabisa...
Spika Ndugai anaagizwa na Jiwe "ku - abuse mamlaka na madaraka yake ya uspika" kwa kukanyaga kanyaga katiba na sheria za nchi mchana kweupe na bila hofu anatenda.
Hii imenitisha sana.
Kila mtu anajua kuwa CHADEMA ni chama cha siasa halali kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi yetu. Kina katiba na utaratibu wake wa kujiendesha na kujisimamia.
Ndugai na wenzake hasa Magufuli hawaipendi CHADEMA. Lakini kwa yeye Ndugai, sijui anaona taabu gani ingalau kuheshimu hilo tu la uwepo wa CHADEMA kisheria na kikatiba.
Akifanya hivi, na yeye ataheshimika na ataendelea kutenda na kutekeleza majukumu yake ya Uspika hata kama na sisi wengine hatumpendi.
Anamsema mwenzake Mbowe kuwa anatukana wanawake (sijui hata kama ni kweli).
Cha ajabu yeye anatukana na kuonesha dharau ya waziwazi kwa CHADEMA yote, wanachama na wafuasi wake wote mamilioni kwa mamilioni Tanzania na duniani note.
Kwa dharau kabisa Ndugai anapiga propaganda za kijinga kuwa CHADEMA ni kama kampuni ya mtu binafsi..
Mtu mwenye akili anaweza kujiuliza hivi;
Kama CHADEMA ni "kampuni ya mtu binafsi", ina maana hao anaowaita " wabunge" na kusema atawalinda, hajui kuwa watakuwa pale wakiwa na dhamana ya chama hichohicho anachokiita "kampuni binafsi ya mtu?"
Maana siyo kwamba hakitambui chama. Yeye hatambui kufutwa kwao uanachama tu.
Hakika Ndugai haeleweki. Yuko very frustrated.
Baadaye Ndugai ameendelea kusema, hatawatambua hawa kuwa ni "wabunge halali" iwapo tu kutakuwa na "sababu halali za kikatiba..."
Baada ya kusikia hili nikachoka kabisa. Nikajiuliza huku ni kuchanganyikiwa au ni kukosa ufahamu...?
Hivi ina maana Ndugai hajui sifa za kikatiba za mtu kuwa mbunge?
Na je, hivi huyu mzee ina maana hujui pia sifa za mtu kukoma au kukosa uhalali wa kuwa mbunge wa Bunge la JMT ambalo yeye ndiye kiongozi wake...?
Ningemwona wa maana sana kama angewashauri kina mama hawa kutumia njia za kisheria kudai haki yao ya uanachama (kama wanadhani au ona kuwa wameonewa) ndani ya chama au mahakama..
Lakini anachotenda Spika ni mbaya sana. Anaacha precedence mbaya sana kwa watoto wetu na mfumo wetu wa utawala...