Video: Tazama Maafisa usalama walivyomdhibiti mtu aliyetaka kumvamia Rais Museven

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Askari wa Usalama wanaomlinda Rais wa Uganda Yoweri Museveni walimzuia mwanaume asiyetambuliwa aliyekuwa akijaribu kumkaribia Rais Museveni katika viwanja vya Msikiti wa Mbogo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea wa NRM, Faridah Nambi anayewania ubunge katika jimbo la Kawempe Kaskazini.

Dhamira ya mwanaume huyo aliyekuwa amevaa fulana yenye picha ya Mtoto wa Kwanza wa Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba haikujulikana kama alikuwa na nia ovu au kwa mapenzi alitaka kumkumbatia Rais wake.

Mkutano huo umefayika jana Machi 11, 2025 katika jimbo la Kawempe Kaskazini ambapo Nambi anashindana na wagombea wengine kumi ili kupata atakaerithi kiti cha mbunge aliyefariki Muhammad Ssegirinya’s
Your browser is not able to display this video.
 
Kuna huyo jamaa aliyetokea upande wa Kulia, apewe Kongole namna alivyoweza kumuwahi huyo raia Mvamizi

Sasa jamaa ataenda kuwajibu vizuri PSU maswali yao

Otherwise, anaweza asionekane tena
 
Haka kavideo kamenifunza jambo ... kumbe kwenye hiyo kadamnasi ya watu kuna "wadau" waliovalia kiraia ,tena tisheti za chama tawala Uganda af huwezi wadhania , sio mbaya.😅😅😅... ila huyo jamaa kajichanganya sana ...THEY( PRESIDENTIAL PROTECTION UNIT)WILL GOING TO HAVE LITTLE SESSION WITH HIM.
 
Watamuachia tu baada ya kubaini hakuwa threat kwa kaguta Mu7.. kama alikuwa na lake jambo basi he will suffer terribly 😔
Ukimbelembele huo haya yamemgeukia ,anyway watamuChia tu

Ova
 
Ñakumbuka jinsi marehemu Ali Hassan Mwinyi alivyopigwa Kibao na Katoto Ka Kiislam kenye msimamo mkali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…