Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Ni Mch. Eliona Kimaro wa kanisa la K.K.K.T - DSM akimwaga madini adimu sana.
Anasema, viongozi wengi wa nchi za Kiafrika ni wabinafsi na huogopa sana watu wenye akili (talented people) kwani badala ya kuwalinda na kuwaweka karibu watu hawa ili kuwatumia kusaidia uwepo wao kwenye iti vyao vya madaraka ya kisiasa, wao huwaona kama ni tishio (threat) la viti vyao.
Hivyo hufanya kila aina ya fitna ili kuwaweka mbali watu hawa wakidhani kuwa hiyo ndiyo salama ya nafasi zao hizo za kisiasa...
Bahati mbaya wasichokijuia ni kuwa, mara nyingi hawa watu talented huwa hawana haja na permanent positions. Mungu huwaweka mahali fulani kwa kusudi maalumu na la muda maalumu tu.
Anatolea mfano mfano wa Yusufu aliyekuwa na karama ya kipekee na kutumiwa vyema na Farao wa Misri ya Kale kuliepusha taifa zima ktk baa la njaa.
Farao hakumwogopa Yusufu. Alimvuta karibu na kutumia ujuzi na maarifa yake kuliokoa taifa lote..
Huwezi kuongoza taifa la watu wenye njaa.