MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Siku zote Watanzania humu JF hutuambia wao hawataki kuongea Kingereza kisa ni cha wakoloni, kwamba watakomaa na Kiswahili, ila mimi husema ziku zote humu, ni uzembe na uvivu wa kutokutaka kuchosha akili kwenye kujifunza lugha, hamna cha uzalendo wala utumwa wala ukoloni wala nini maana hata Kiswahili wanachojivunia huwa kinawapa matatizo haswa ikija kwenye matumizi rasmi ya kiuandishi na elimu.
Pia ukifuatilia hata uandishi wao humu, utaona matatizo makubwa sana, hamna lugha hata moja wanayoimudu ipasavyo.
Tazama hii video, jamaa amewaibukia wanafunzi wengi chuo kikuu cha Dodoma na kila mmoja ameshindwa nini maana ya neno 'tarakimu', yaani mwanafunzi amesoma chekechea akamaliza, akamaliza shule ya msingi, akapitia shule ya upili hadi kidato cha nne, akaendelea na kumaliza kidato cha sita na hatimaye akajiunga chuo kikuu, lakini neno la msingi kwenye shughuli za elimu linamshinda, halafu huyo ndio utakuta anahitimu shahada ya uhandisi na kuingia kitaa kusaka ajira.