Uchaguzi 2020 Video: Wananchi Same waandamana kupinga jina la mgombea waliloletewa na CCM

wengine hawa hapa
 
Sasa kwa kuwa hawakubaliani na maamuzi husika na kuona wamedharauliwa ndiyo na wao waonyeshe nguvu yao hivyo kuchagua upinzani.
Haya maamuzi toka juu, yatawapa faidi kubwa Sana upinzani.

Maana Wanachama Wana maamuzi yao na Mwenyekiti ana maamuzi yake.
 
Wajumbe siyo wa watu wa kubeza namna hiyo . Naitambua nguvu yao ivyo wasikilizwe na wasichaguliwe kiongozi waachwe wachague wamtakaye.
 
Wanabishana na maamuzi ya vikao vya chama?..!!.
Kamata weka ndani
Kwa hiyo viongozi ndio wenye haki zaidi kuliko wananchi...halafu mtu mwenyewe ameongoza miaka 15 anarudishwa wa nini...ni kufuga ugonjwa tu.
 
Tatizo la watani zangu ni ulimbukeni, kwani lazima diwani atokane na ccm? kama mtu wenu hakubaliki huko ccm si muangalie upande wa pili.
 
Tunaomba sana mawazo ya wananchi yaheshimiwe ,Ccm tuwe makini sana tusije poteza kata
 
Kazi imeanza
 
Sasa kwa kuwa hawakubaliani na maamuzi husika na kuona wamedharauliwa ndiyo na wao waonyeshe nguvu yao hivyo kuchagua upinzani.
Ninachokiona hapo kwa hali yoyote ile, iwe jina litarudi wanalotaka au libaki hilo hilo wapinzani wana 'kura za faida'.

Sababu akiletwa yule aliyeshinda kura za maoni bado hawa wengine watamkataa kwenye box kuwakomoa wenzao wanaoshangilia kabla mtoto hajalia.
 
Wajumbe tunaendelea kuwakataa wote Waliopita kimazaBe
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…