Video: Wananchi wa Chandama, Wilaya ya Chemba, Dodoma wakichimba na kutafuta maji ambayo sio safi na salama

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Kama mnavyoona hapa, wananchi wanachimba na kuchota maji kwenye mto uliokauka. Eneo hili linadaiwa kuwa ni Chandama, Wilaya Chemba, Mkoa Dodoma

Video hii inasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Kada wa CHADEMA Martin Maranja Masese ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram:

"Hawa ni Watanzania wanatafuta maji kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku. Siyo maji ya viwanda. Maji kwa matumizi ya nyumbani.

Unaweza kufikiri Tanzania ndiyo imepata uhuru wake jana, kumbe ina miaka 65 ya uhuru. CCM imewafanya Watanzania kuishi kama wapo vitani. Tanzania ina kilomita za ujazo (km³) 96 za rasilimali za maji tamu zinazoweza kurejelewa kila mwaka (renewable freshwater resources). Tanzania ina maziwa makuu matatu (Tanganyika, Victoria, Nyasa).

Tanzania inapata mvua za kitropiki mara mbili kwa mwaka. Tanzania ina mito mingi ya kudumu na ya msimu pamoja na hifadhi kubwa za maji chini ya ardhi (groundwater). Tanzania ina mabonde makuu tisa ya maji (river basins). Lakini Watanzania hawana maji safi na salama kwa matumizi yao"


Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…