Tatizo TBC hawataki ku stream LIVE online (youtube na kwenye website yao) lakini kuna wenzetu wazalendo wameirekodi na kuiweka online ili wengine wapate kuona mijadala inavyooendelea mle ndani.
Nimeona bora ni share nanyi
dakika 30 za mwanzo zinaonyesha kuwa pamoja na mapungufu ya bunge hili la katiba, nadhani liko more entertaining kuliko bunge la kawaida
Kuna haja ya kuwa na kanuni kwamba ili jambo au hoja ipite ni lazima ikubaliwe na angalau 50% ya kila kundi. Si makundi yanayotuwakilisha Bungeni yanajulikana? Basi hiyo kanuni itungwe fasta na itakuwa imekata ngebe za CCM kutegemea wingi wao kama turufu ya kuburuza wengine.