SI KWELI Video ya Mbowe akimpongeza Rais Samia kwa maridhiano ni ya mwaka huu (2024)

SI KWELI Video ya Mbowe akimpongeza Rais Samia kwa maridhiano ni ya mwaka huu (2024)

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Screenshot 2024-12-04 092153.png



 
Tunachokijua
Freeman Aikaeli Mbowe ni Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amewahi kuwa mbunge wa Hai na mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Chama amekuwa akikutana na kadhia mbalimbali ikiwemo kufikishwa mahakamani mara kadhaaa na hata kukaa mahabusu.

Samia Suluhu Hassan ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania aliyeanza uongozi wake mwaka 2021, March mara baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa awamu ya tano Daktari John Pombe Magufuli kufariki dunia na hivyo makamu wake wa rais kuchukua nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Julai 21, 2021 Mbowe alikamatwa na jeshi la polisi akiwa jijini Mwanza na baadaye akasafirshwa hadi Dar es salaam na kisha kusomewa mashitaka matatu ikiwemo la ugaidi. Kesi ilichukua miezi kadhaa kabla ya muendesha mashtaka wa serikali kusema kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo jambo lililopekea Mbowe kuachiwa huru na wenzake March 4, 2022.

Mbowe baada ya kuachiliwa huru March 4, 2022 alienda ikulu ambapo alikutana na Rais Samia walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kushirikiana katika kuijenga Tanzania yenye misingi ya haki na kuheshimiana.

Tarehe 3-12-2024 kumekuwepo na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii kikimuonesha Mbowe akimpongeza Rais Samia kwa kurishia maridhiano huku ikiwa imeambatana na jumbe (captions) mbalimbali. Tazama hapa na hapa

Uhalisia wa video hiyo upoje?

Ufuatiliaji kwa njia ya kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo ni halisi na ni kweli kuwa Mbowe alimpongeza Rais Samia kwa kuridhia maridhiano. Lakini ufuatiliaji umebaini kuwa licha ya kuwa video hiyo ni halisi lakini siyo ya mwaka huu (2024) na badala yake imekuwepo mtandaoni kuanzia mwaka 2023.

Chaneli ya Youtube ya SAUT DIGITAL walichapisha video katika mtandao huo 21-01-2023 ambayo ilikuwa ikielezea kuwa CHADEMA imefanya mkutano jijini Mwanza kwa ajili ya kuzindua mikutano ya hadhara iliyokuwa imezuiliwa kwa muda mrefu. Ambapo katika video iliyoeleza taarifa hiyo kipo pia kipande cha video ya houtua ya Mbowe aliyoitoa katika mkutano huo kwa kueleza kuwa;

“Nasimama mbele ya jamii ya Mwanza na mbele ya dunia Kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavo alikuwa mvumilivu kwenye vikao vingi mfulululizo tulivyofanya naye nikimshawishi atambue kwamba hii nchi inahitaji maridhiano”.

Lakini pia video hio ilichapishwa katika mtandao wa Facebook na ukurasa wa Mama Yuko Kazini tarehe 21-01-2023 huku wakiweka na ujumbe ulioeleza kuwa Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa utayari wake wa kuleta maridhiano.

Hitimisho

Video hiyo ni halisi na Mbowe aliyatamka maneno hayo lakini si ya hivi karibuni bali ni ya Januari 1, 2023 alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara jijini Mwanza.
Back
Top Bottom