- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Naomba msaada wa kuhakiki video hii kama ni ya kweli au imetengenezwa
- Tunachokijua
- Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Video ya ng'ombe anayeendesha baiskeli iliwekwa mtandaoni tangu Julai 26, 2024 katika mtandao wa Instagram kwenye akaunti inayoitwa Sirwan.Maghded tazama hapa.
Upi ukweli wa taarifa hii?
Katika kufuatilia ukweli wa taarifa hii JamiiCheck iliichapisha video hii kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii ambapo asilimia 90 ya wadau walieleza kuwa video hiyo si halisi na imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence). Wadau hapo wa Mitandaoni walitoa vigezo mbalimbali vinavyoifanya video ya ng'ombe kuwa ya Akili Mnemba:
Mathalani, Mdau wa Instagram anayetumia jina la Sharman_smn alieleza kuwa video hiyo si halisi na imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba. Katika kufafanua zaidi hoja hii Sharman_smn ametoa hoja 6 zifuatazo:
Video hii ni feki kwa sababu1. Miguu ya nyuma nayo inazugusha pedal wakat hakuna kitu hicho kweny hiyo baiskeli, Usukani unatengana na main body katika muda fulani hivi. Huyo ng'ombe ana miguu mitatu tu, mguu wa nyuma upande wa pili wa baiskeli hauonekani, 4. Baiskeli haina kibao cha kukalia au kimingia tumboni?Hakuna uwiano wa uzito wa Ng'ombe na uwezo wa baiskeli baiskeli, kimuonekano Baiskeli hiyo ni ya kawaida ya kutembelea ambapo wastani wa uzito inayiweza kuhimili ni 140kg, ng'ombe wa muonekano huo haapungui 600kg, so baiskeli haiwezi kusupport uzito huoKwa kipengele hicho hicho cha uwiano wa uzito na uwezo wa baiskeli kuhimili uzito, Hata kaka baiskeli ingeweza kubeba uzito huo basi magurudumu yake yasingeweza kuzunguka kwa speed hiyo, mwendo ungekuw wa kudorora sana na kungekuwa na ugumu wa kuepush pedals. Mambo ni mengi ila nafasi ya kuandika haitoshi. Ila Kwa ufupi hiyo ni video iliyozalizalishwa na akili mnemba (AI)Maoni ya Sharman_smn hayotofautiano na wadau wengine ambao nao wanakuballiana video hiyo sio halisi bali imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Mnemba. Baadhi ya maoni hayo yatazame kwenye picha hapa chini:
Nini mtazamo wako kuhusu majibu haya ya wadau wa JamiiCheck?