Video ya vijana wawili hodari imepata tuzo

Video ya vijana wawili hodari imepata tuzo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Imekuwa kawaida sana siku hizi vijana katika media kunipigia simu na kuniombawanifanyie mahojiano kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Siku moja kijana Masekepa Asangama alinipigia simu na kuniomba aje nyumbani kwangu ana jambo anataka tuzungumze.

Katika mazungumzo yetu kitu kimoja kilinivutia nacho ni kule yeye kuwa ananisikiliza anaandika ananisikiliza anaaandika.

Angalia picha ameshika note book.
Hapo hapo nikajua huyu kjana ni makini katika kazi yake.

Masekepa alitaka sana kujua historia ya Bi. Titi Mohamed na kaina mama wengine waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Nikamfungulia Maktaba na kumpa picha za akina mama hawa.
Haukupita muda akaja nyumbani na mwenzake Abdallah Kurwa wakaja sasa rasmi kwa mahojiano.

Muda ukapita nami nikwa nimesahau.

Leo jioni Masekepa kanipigia simu kunifahamisha kuwa video waliyotengeneza imepata ushindi wa kwanza.

Kaniletea video na kwa kweli nimeipenda.

Naamini na wewe itakufurahisha pia.

Video hii imetumia picha nyingi kutoka Nyaraka za Sykes na picha nilizopewa na watoto wa Ali Msham.

Katika video hii kuna picha ya mtoto wa Bi. Titi Halima anazungumza kwa ufasaha ule ule wa marehemu mama yake akieleza mambo yalivyokuwa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Picha hii Halima ana umri wa kiasi miaka saba hivi.

1656622872084.png

(Picha kwa hisani ya watoto wa Ali Msham)​

Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la Magomeni Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar wa tano Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi wa saba Mama Tindwa waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na wa tatu ni Bi. Titi Mohamed na pembeni ni mwanae Halima na baada ya mwanae ni Bi. Tatu biti Mzee.

1656623632352.png

Mtoto wa Bi. Titi Mohamed Bi. Halima Mzee kama alivyo hivi sasa​
 
Back
Top Bottom