Vidume mtremko!!

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2009
Posts
2,469
Reaction score
284
Wadau..
inakuaje siku hizi baadhi ya wanaume(mabachela)..hasa waliojaaliwa kismati(mvuto au chochote kile) cha kupendwa... wankuwa wavivu wa kufanya kazi kwa bidii.. wanakuwa tegemezi ..hasa kiuchumi kwa wanawake?!

Wengine huwa jasiri hadi kuandika mitandaoni kujinadi kwa sifa ya kuwa na uwezo wa ku-care(wakati hana mbele wala nyuma)...!!

Binafsi..yanisikitihsha hali hii.. naamini mwanaume yabidi ujitengenezee nafasi yako mwenyewe katika jamii(wenye hekima zao wanatambua)!!:embarrassed1:
 
Hata waliooa.sio mabachela tu.Wengi siku hizi ni wanaume BUSHOKE.Wanataka kulishwa.Na wanamuziki wa kikongo ndio wamezidi
 
Ukiona hivyo na uanze kutia shaka sana na uanaume wa mtu huyo!...Aidha anazidiwa na hormones za kike au ana biashara zingine haramu...Tangu lini mwanaume akajinadi bana?
 
Ukiona hivyo na uanze kutia shaka sana na uanaume wa mtu huyo!...Aidha anazidiwa na hormones za kike au ana biashara zingine haramu...Tangu lini mwanaume akajinadi bana?
Hata humu JF wapo sana.Ila nsiniquote vibaya,sijasema wote,nimesema baadhi wapo humu JF.
 
Hapo kwa redi ZD....uzoefu??
Hapana.sio uzoefu.Si unajua magazeti tena ya uwazi na risasi.Yanaweka mambo bayana kabisaaaaaa.Na hata hivyo mie sina uwezo wa kumlisha mwanaume.Najitosheleza mwenyewe tu..
 
Please!!!!!!!!! Of all the places? Not JF!

ZD: kuna watu wameshatangaza nia?
Sio hivyo.Lakini hata wewe ni shahid jinsi post za watu zinavyokuwaga ,kibushokebushoke tu.Haina hata haja ya kuuliza,mtu utamjua tu kama ni wa KIUME au MWANAUME.Sio wote ni magreti sinkaz wengine ni magreti stinkas
 
Ni kizazi kisicho na mwelekeo!

Hata uvaaji wa suruali wa vijana wa kiume unaacha maswali mengi kichwani mwangu: BUT on the other hand - Wanawake wameishiwa aibu - wanatongoza vijana wakiume than ever before - Jamii nzima nadhani imebadilika na imehalalisha kila kitu
 
Sio hivyo.Lakini hata wewe ni shahid jinsi post za watu zinavyokuwaga ,kibushokebushoke tu.Haina hata haja ya kuuliza,mtu utamjua tu kama ni wa KIUME au MWANAUME.Sio wote ni magreti sinkaz wengine ni magreti stinkas
Hahaha naona leo umeamua kuwatolea uvivu!
 
Ukiona hivyo na uanze kutia shaka sana na uanaume wa mtu huyo!...Aidha anazidiwa na hormones za kike au ana biashara zingine haramu...Tangu lini mwanaume akajinadi bana?

Veterani ..upo?! au ulienda tangaza uvuvuzela jimboni?!!:smile-big:
 
Si wanataka kuolewa na wanawake ila wajiandae kulea watoto au hujui siku hizi wanawake nao wana wowa:becky::becky::becky::becky:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…