Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Wakuu salaam, tunaendelea na mada kuu ya aina za maneno katika lugha. Katika uzi huu tutafafanua dhana ya Vielezi na aina zake. Twende pamoja:
VIELEZI
Vielezi ni maneno yanayotumika kufafanua kitenzi, kivumishi au kielezi kingine. Au pia, ni maneno yanayosifu au kufasili sura za vitenzi, vivumishi au vielezi vingine.
Vielezi vinapotumika kufafanua vitenzi
1. Vielezi vya namna
Hivi huonyesha namna kitendo kinavyotendeka. Hujibu swali “vipi?”. Kwa mfano, nyanya alitembea taratibu.
2. Vielezi vya mahali
Hivi huonyesha mahali kitendo kinapotokea au kutendeka. Kwa mfano, mama alikwenda sokoni. Alipanda Juu ya mti akaangua machungwa.
3. Vielezi vya wakati
Hivi hueleza wakati wa kutendeka kwa kitendo. Kwa mfano, alichapisha kitabu chake mwaka jana.
4. Vielezi vya idadi
Vielezi hivi hueleza kiasi cha kutendwa kwa tendo flani. Pia vielezi hivi huonyesha ni mara ya ngapi katika safu kitendo kimefanyika. Kwa mfano, ameenda sokoni mara tatu leo.
5. Vielezi viigizi
Vielezi hivi huiga jinsi kitendo kilivyotendwa. Hufafanua vitenzi kwa kufuatanisha mlio baada ya kitendo kutendeka. Kwa mfano, mtoto alilala fofofo!
6.Vielezi viulizi
Vielezi hivi huuliza juu ya tendo. Kwa mfano, utakuja lini kututembelea?
7. Vielezi vioneshi
Hivi hutumiwa kuonyesha mahali tendo lilifanyika. Kwa mfano, alienda pale kununua viazi.
Pia Soma:
Credit kutoka vitabu:
- Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006
- Kimani Njogu, Alice Mwihaki na Aswani Buliba, Sarufi ya kiswahili: uchanganuzi na matumizi: Jomo Kenyatta Foundation 2006.
- Jamvi la Uhakiki wa Kiswahili

- Mtoto yule alianguka vibaya.
- Chakula alichopika mama ni kitamu sana
- Mpishi yule alipika chakula vizuri sana
1. Vielezi vya namna
Hivi huonyesha namna kitendo kinavyotendeka. Hujibu swali “vipi?”. Kwa mfano, nyanya alitembea taratibu.
2. Vielezi vya mahali
Hivi huonyesha mahali kitendo kinapotokea au kutendeka. Kwa mfano, mama alikwenda sokoni. Alipanda Juu ya mti akaangua machungwa.
3. Vielezi vya wakati
Hivi hueleza wakati wa kutendeka kwa kitendo. Kwa mfano, alichapisha kitabu chake mwaka jana.
4. Vielezi vya idadi
Vielezi hivi hueleza kiasi cha kutendwa kwa tendo flani. Pia vielezi hivi huonyesha ni mara ya ngapi katika safu kitendo kimefanyika. Kwa mfano, ameenda sokoni mara tatu leo.
5. Vielezi viigizi
Vielezi hivi huiga jinsi kitendo kilivyotendwa. Hufafanua vitenzi kwa kufuatanisha mlio baada ya kitendo kutendeka. Kwa mfano, mtoto alilala fofofo!
6.Vielezi viulizi
Vielezi hivi huuliza juu ya tendo. Kwa mfano, utakuja lini kututembelea?
7. Vielezi vioneshi
Hivi hutumiwa kuonyesha mahali tendo lilifanyika. Kwa mfano, alienda pale kununua viazi.
Pia Soma:
- Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili
- Aina za Nomino (N) katika Lugha Kiswahili
- Aina za Vitenzi (T) katika lugha ya Kiswahili
- Aina za Viwakilishi (W) katika lugha ya Kiswahili
Mwakisyala Signed