#COVID19 Vietnam: Afungwa miaka mitano kwa kusambaza Virusi vya Corona

#COVID19 Vietnam: Afungwa miaka mitano kwa kusambaza Virusi vya Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanaume mmoja huko Vietnamese amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kosa la kukiuka masharti dhidi ya kujikinga na Covid-19 na kusambaza virusi vya Corona.

Mahakama imemkuta na hatia bwana Le Van Tri kwa kusambaza maambukizi ya ugonjwa hatari kwa watu nane , ambapo mmoja tayari amefariki.

Mpaka hivi karibuni Vietnam imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa kuweka masharti makali dhidi ya corona.

Lakini maambukizi yameongezeka tangu Juni, na kuzidi zaidi katika kuibuka kwa kirusi aina ya Delta.

Taifa hilo lina wagonjwa wa Covid 19 zaidi 530,000 vifo 13,300 , na vingi vilitokea miezi michache iliyopita.

Wagonjwa wengi wa Covid wako mji mkuu wa Ho Chi Minh .

Mwanzoni mwa mwezi Julai , Tri, mwenye umri wa miaka 28, aliripotiwa kusafiri kwa kutumia pikipiki kutoka mji wa Ho Chi Minh mpaka jimbo la Ca Mau kusini mwa nchi hiyo.

Huko Ca Mau, Tri alibainika kudanganya kuhusu hali yake ya kiafya alipoulizwa kuhusu historia ya safari zake na pia kushindwa kufuata sheria zilizowekwa.

Mamlaka nchini humo iliweka masharti kuwa yeyote anayesafiri kwenda jimbo lingine anajitenga kwa muda wa siku 21.

Baadae Tri alipimwa na kukutwa na Covid, na akakutwa amesambaza kwa wanafamilia yake pamoja na wafanyakazi wa kituo cha ustawi alichotembelea.

Tri amehukumiwa kifungo na kupewa faini ya dola $880 (£630).

BBC Swahili
 
Bongo sie tumekazania kuambiana kuchanja tu ila kuambukizana ni ruksa ndio maana tunakusanyana bila tahadhari ili tuambiane tukachanje.
 
Back
Top Bottom