Vietnam na historia yake kwenye vita

Vietnam na historia yake kwenye vita

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Historia

Milki jirani ya China

Vietnam ilitawaliwa kwa karne kadhaa kutoka China. Athira ya kiutamaduni ya China ilibaki muhimu hata katika uhuru.

Katika karne ya 18 nchi iliunganishwa chini ya makaisari wa Hue.

Koloni la Ufaransa

Athira ya Ufaransa ilikua na kati ya miaka 1858 na 1883 utawala wa nchi ulichukuliwa na Ufaransa. Kusini mwa nchi kulikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Cochinchina. Annan (eneo la Vietnam ya Kati) na Tongking (kaskazini) zilikuwa nchi lindwa chini ya utawala wa kaisari wa Hue lakini hali halisi mamlaka ilikuwa mikononi mwa Ufaransa.



Vita ya ukombozi

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Vietnam ilitwaliwa na Japani iliyoacha maafisa Wafaransa wa serikali ya Víchy ofisini lakini kushika utawala wa juu.

Kundi la Viet Minh walioongozwa na mkomunisti Ho Chi Minh waliwapinga kwa njia ya vita ya msituni.

Mwaka 1945 Japani ilijaribu kutumia Wavietnam upande wake ukaondoa Wafaransa madarakani na kumtangaza Kaisari Bao Dai wa Hue mtawala wa Vietnam huru.

Lakini baada ya miezi michache vita ikaisha na Ho Chi Minh alitangaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam mjini Hanoi. Wafaransa wa serikali ya Paris walijaribu kujenga uhusiano naye lakini baada ya kurudi walilenga kuchukua utawala upya.

Vita ya kupigania uhuru ilifuata hadi mwaka 1954 Ufaransa ikashindwa.

Kipindi cha Vietnam mbili

Vietnam iligawiwa katika Vietnam Kaskazini na Vietnam Kusini. Jeshi na watawala wa kikoloni wa Ufaransa waliondoka kabisa. Wavietnam wengi wa kaskazini, hasa Wakristo, walioogopa serikali ya kikomunisti walikimbilia kusini.

Lakini uchaguzi huru uliokubaliwa huko Geneva haukutekelezwa kwa sababu serikali za kidikteta za kusini zilikataa.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilianzishwa na wakomunisti wa kaskazini waliosaidiwa na China na Umoja wa Kisovyeti dhidi ya serikali ya kusini iliyopata msaada wa Marekani.

Kaskazini kuteka Kusini na kuunganisha taifa

Katika vita ya Vietnam majeshi ya Marekani na Vietnam Kusini yalishindwa.

Tarehe 30 Aprili 1975 jeshi la Vietnam Kaskazini ilitwaa mji wa Saigon. Nchi yote iliunganishwa kama Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam tarehe 2 Julai 1976.

Watu kwa idadi


Kwa jumla kuna wakazi milioni 86.5

Wengi (85.7%) ni Waviet. Wengine ni wa makabila madogomadogo 54 ambayo hakuna linalofikia 2%.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiviet.

Upande wa dini, siasa ya ukomunisti inabana uhuru. Kadiri yake 18.2% tu za wakazi wamejiandikisha kufuata dini fulani, wakiwemo Wabuddha (7.9%), Wakatoliki (6.6%), waumini wa Hòa Hảo (1.7%), Wakaoda (0.9%) na Waprotestanti (0.9%), kumbe wengine wote hawamuamini Mungu.

Lakini utafiti kutoka nje unataja namba tofauti, hasa kwa dini za jadi, kwamba zinafuata na 45.3% za wakazi wote, na kwamba wasio na dini yoyote ni 29.6%.

Uchumi wa Vietnam

Kati ya miaka 1940 na 1975 Vietnam ilikuwa na kipindi kirefu cha vita ikaonekana kama nchi maskini sana.

Tangu miaka ya 1980 uchumi umesonga mbeleː sasa ni kati ya nchi kwenye njia ya maendeleo zenye uchumi imara sana unaokua haraka.
 
Bila manyanyaso na kutandikana wenyewe kwa wenyew hakunaga maendeleo.
Hayo mataifa makubwa yote walipitia ushenzi wa kuuwana na ndio maana wanaheshimiana hadi leo hii wamekuwa super power.
 
Bila manyanyaso na kutandikana wenyewe kwa wenyew hakunaga maendeleo.
Hayo mataifa makubwa yote walipitia ushenzi wa kuuwana na ndio maana wanaheshimiana hadi leo hii wamekuwa super power.
Japo kuuana wenyewe sio kuzuri lakini kunasaidia kufikisha taifa mahali husika kimaendeleo
 
Back
Top Bottom