JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kwa ajili ya kujifungua salama, andaa vifaa vifuatavyo: -
Sabuni na maji kwa ajili ya kunawa mikono mara kwa mara, kumsafisha mama, na kusafisha vifaa tiba. Vilevile andaa beseni au bakuli kwa ajili ya kunawia na kupokea kondo la nyuma.
Viwembe vipya au mkasi wenye makali kwa ajili ya kukata kiunga mwana.
Dawa kwa ajili ya kusimamisha uvujaji damu.
Nunua boksi dogo la glovu (surgical gloves) kulinda afya ya mama, mtoto na mkunga.
Kamba zilizotakaswa na dawa au kuchemshwa, au riboni au kibanio maalum kwa ajili ya kufunga au kubana kitovu. Zinapatikana duka la dawa.
Andaa kanga, blanketi la watoto wachanga, nepi, n.k. kwa ajili ya kumfuta na kumfunika mtoto ili apate joto la kutosha punde tu atakapozaliwa.
Aidha, unashauriwa unapokwenda kliniki hakikisha unaulizia mahitaji muhimu na vifaa vya kuandaa kwa ajili ya kujifungua ili kuepusha usumbufu hapo baadaye.