Vifaa vya Ujenzi havijashuka bei

Vifaa vya Ujenzi havijashuka bei

Ruyama

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2019
Posts
367
Reaction score
563
Cement bado elfu 16 mfuko mmoja nondo bado elfu 21. Waziri wa Fedha alisema material ya ujenzi yanayo zalishwa ndani yatashuka bei tarehe 1/7 lakini bado bei iko vile vile.

Kwa namna hii ujenzi utakuwa mgumu[emoji134]
 
Tulia mkuu, je ukijenga nyumba tetemeko likapita nayo? Kula bia maana umeshushiwa bei.
 
Ndugu nakushangaa eti unalalama cement bei kubwa 16 elfu? Hujajua bei zahuku mikoani matakoni mwanchi? 20 elfu!
 
Mkuu!

Serikali yako inathamini sana ulevi kuliko masuala ya maendeleo! Inaskitisha kuona kodi kwenye vileo imeshuka lakini upande wa mafuta na ujenzi badala ya kushuka ndo Kwanza znapanda kwa kasi.
 
Mafuta yamepanda bei hakuna kitakachopungua, sana sana vingine vitapanda
Mama anaupiga mwingi!

Katoa nchi kwenye mikono ya chuma ulete sasa tuko vizuri! Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Endeleeni kusikiliza propaganda. Huyo anaeuza cement anategemea mafuta kukufikishia ulipo. Mafuta yapande bei halafu cement ishuke! Je gharama nyingine za uzalishaji zimepungua bei?
 
Hii solidarity fund inakusanywa hadi kwenye vifaa vya ujenzi? basi twafwaaaa.......
 
Na kupanda huku kwa mafuta, sidhani kama vitu vitashuka bei...
 
Back
Top Bottom