Vifaranga vya kuku viwekewe majiko ya kuvipa joto hadi umri gani?

Vifaranga vya kuku viwekewe majiko ya kuvipa joto hadi umri gani?

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Ndugu wanajf na wafugaji wa kuku, hivi vifaranga vinatakiwa viwekewe chanzo cha joto hadi vifikishe umri upi?
 
Ndugu wanajf na wafugaji wa kuku,hivi vifaranga vinatakiwa viwekewe chanzo cha joto hadi vifikishe umri upi?
Inategemea na Hali ya hewa eneo ulilopo ila mara nyingi week nne tu vinakua na manyoya ya kutosha
 
Ndugu wanajf na wafugaji wa kuku,hivi vifaranga vinatakiwa viwekewe chanzo cha joto hadi vifikishe umri upi?
Chanzo cha joto, huwekwa kwa vifaranga sababu kubwa ikiwa kuwaepusha na baridi kwa sbb kwa umri wao wanakuwa hawana manyoya ya kutosha ya kufanya waweze kuhimili baridi wenyewe.

Kwa hivyo mara nyingi tunaweka vyanzo vya joto kwa vifaranga mpaka pale tutakapoona sasa manyoya ya kutosha yameshatoka na kuku anaweza kuhimili baridi mwenyewe.

Kwa hiyo mara nyingi huwa hadi wiki ya 2 siku 14 tayari kuku anakuwa ashapata manyoya ya kutosha. ingawa unaweza kuongeza ka muda kidogo. lakini gharama za mkaa au gesi zinatutafuna sana wafugaji tunaona hapa hapa inatosha.
 
Asante kwa ushauri!Nitaufanyia kazi
 
Unaweza kuniambia kuku wako dawa ya nafua unatumia ipi?
 
Back
Top Bottom