KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 540
baada ya ya post yangu ya vilio na kusaga meno vya tawala ngome ya chadema pale mlimani, kuna watu walidiriki kusema mimi nia yangu ilikuwa mbaya kutoa taarifa ile eti nafurahia watu kukosa haki yao ya kupiga kura. Ukweli ni kuwa post ile ilisaidia sana watu wengi kutoa mawazo yao ya nini kifanyike ili kuwasadia watu wasipoteze haki yao ya kupiga kura. Wengine wenye influence walikwenda mpaka tume ya uchaguzi ili itoe taarifa sahihi kwa wa piga kura. Hivi ninavyoandika kwenye mbao za majina limebandikwa tangazo linalowataarifu watu kuwa kama ulipigia kura Nkuruma na jina hulioni, basi nenda kwenye kituo cha shuleni au Kafteria huko utalikuta, kitu ambacho hapo awali hakikufanyika. Watu wengi ambao walianza kukata tamaa kuwa ndoto zao za kuleta tumaini jipya zimepotea hivi sasa wanashangilia baada ya kuyakuta majina kwenye vituo vingine.
pendekezo: tuhakikishe na kwenye vituo vingine taarifa za wapi majina yanaweza kupatikana zibandikwe (kama hazijabandikwa) kwenye vituo hivyo ili kuwarahisishia watu utafutaji wa majina
pendekezo: tuhakikishe na kwenye vituo vingine taarifa za wapi majina yanaweza kupatikana zibandikwe (kama hazijabandikwa) kwenye vituo hivyo ili kuwarahisishia watu utafutaji wa majina